Na Charles James, MICHUZI TV

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na Taasisi binary katika kukuza na kuendelea vipaji vya watoto mashuleni ili kuinua sekta ya Michezo nchini.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe Edward Mpogolo wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi wanne wa kituo cha Michezo cha Fountain Gate wanaokwenda nchini Norway kushiriki mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 10 hadi 19.

Mhe Mpogolo amesema wao kama Serikali ya Wilaya ya Dodoma wanathamini mchango mkubwa unaofanywa na Fountain Gate katika kukuza michezo kwa vijana wadogo ambao watakuja kuwa msaada mkubwa kwa Taifa Siku zijazo.

" Sisi kama Wilaya ya Dodoma tunajivunia kazi kubwa sana inayofanywa na wenzetu wa Fountain Gate, wamekua na mchango usiyotiliwa shaka katika ujenzi wa mchezo. Ni lazima kama Wilaya tuwaunge mkono na tayari tumeshawapa eneo kubwa zaidi kwa ajili ya kujenga akademi kubwa yenye kubeba vijana wengi zaidi.

" Chini ya Rais Magufuli kila mtu amejionea namna ambavyo Serikali imewekeza nguvu kubwa kwenye michezo, na hii ni kwa sababu tunaamini sekta hii inatoa ajira kwa kundi kubwa la vijana lakini ni sekta ambayo inatumika kutangaza Nchi yetu," amesema Mhe Mpogolo.

Aidha DAS Mpogolo amewataka vijana hao wanaokwenda kushiriki mashindano hayo kutumia fursa hiyo kutangaza Nchi pamoja na vivutio vinavyopatikana ikiwemo Mbuga za Wanyama na Mlima Kilimanjaro.

Amewataka kuonesha uzalendo, nidhamu na kutokata tamaa wanapokua kwenye mashindano yao kwani watanzania wako nyuma yao wakiwaombea ili wafanye vizuri na kuiletea Nchi sifa.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Fountain Gate, Japhet Makau ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa namna ambavyo imekua ikiwapa sapoti pamoja katika kuhakikisha vijana wenye vipaji wanalelewa katika mazingira yenye kukuza vipaji vyao.

Wanafunzi waliochaguliwa kushiriki michezo michuano hiyo ni Abiel Renatus Tarimo, Enos Boniface Semela, Brown Vicent Meshack na Abduraziz Beberwa Ahmed na wataambatana na mwalimu mlezi kutoka Fountain Gate Dodoma Sekondari, Lespicius Mwelinde France.

Nafasi hii ni muhimu kwa vijana kuonyesha vipaji vyao na inaweza kuwawezesha kupata 'scholarship' kwenye shule za nje ambazo zinaendeleza soka la vijana.Vijana hawa kutoka Fountain Gate Academy wataungana na vijana wa kituo cha Magnet cha jijini Dar es Salaam kuunda Timu ya Tanzania.

Norway CUP ni mashindano makubwa ya vijana yanayoongoza duniani kwa kuwaleta vijana kutoka pande zote za dunia pamoja. Hadi sasa nchi Zaidi ya 127 duniani na maelfu ya vijana wamepata nafasi ya kishiriki mashindano haya.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, Edward Mpogolo akiwa na vijana wa Taasisi ya Fountain Gate wanaoelekea Nchini Norway kushiriki mashindano ya vijana chini ya miaka 19 na miaka 10.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, Edward Mpogolo akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga vijana wanne wa Taasisi ya Fountain Gate wanaoelekea Nchini Norway kushiriki mashindano ya vijana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...