Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na
Magereza wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya Wizara
yake. Kikao hicho kilifanyika Ukumbi wa Wizara jijini Dodoma, leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimpa hati ya kiapo Afisa
Utumishi wa Wizara hiyo, Andrew Kiangi, kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya
Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya
Utumishi na Utendaji wa Askari wa Majeshi hayo. Tukio hilo lilifanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo jijini Dodoma leo. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu) na Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, wakiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume ya Utumishi
ya Polisi, Uhamiaji na Magereza katika kikao cha kujadili utendaji wa vyombo
vilivyopo chini ya Wizara. Kikao hicho kilifanyika Ukumbi wa Wizara, jijini
Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola
(kulia) akimuapisha Afisa Utumishi wa Wizara hiyo, Andrew Kiangi, kuwa Mjumbe
wa Sekretarieti ya Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji
inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa Askari wa Majeshi hayo,
katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dodoma, leo. Kulia (aliyekaa) ni Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...