MKURUGENZI
wa Maendeleo ya jamii kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia
wazee na watoto, Patrick Golwike,akizungumza wakati wa ufunguzi wa
warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la
Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi kutoka Save the Children Makao Makuu Dar es Salaam Bi.Angela
Makota akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu
ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children
iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Watoto wizara ya Afya Sebastian Kitiku,akizungumza
wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni
iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.
Mratibu wa ufuatiliaji wa Shirika la Save the Children, Kanuty
Munishi,akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa
ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na
Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma. 

Sehemu ya wadau wakifatilia wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini
khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children
iliyofanyika jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Maendeleo ya jamii kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya
jamii jinsia wazee na watoto, Patrick Golwike,akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi kutoka Shirika la Save the Children na wadau mara
baada ya kufungua warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa
na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.







Warsha ya nne ya tathimini na kupinga mila na desturi za mimba na ndoa za utotoni kwa mkoa wa Shinyanga imefanyika leo Julai 16,2019 Makao makuu ya nchi,jijini Dodoma. Akizungumza katika warsha hiyo ya tathmini iliyokutanisha wadau mbalimbali wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga,Kaimu katibu mkuu wizara ya Afya,maendeleo ya jamii,jinsia Wazee na Watoto ,Idara kuu ya Maendeleo Patrick Golwike amesema lengo la warsha hiyo ni mpango mkakati wa kupashana habari na kupambana na mila potofu dhidi watoto .
Golwike
ambaye pia ni mkurugenzi idara ya Maendeleo ya Jamii ametaja baadhi ya
mila na desturi potofu na zenye madhara ambazo zimeshamiri mkoani
Shinyanga ni mimba za utotoni , kumwozesha mtoto wa kike mapema kwa
tamaa ya kupata ng’ombe huku akibainisha kuwa mkoa wa Shinyanga ukishika
nafasi ya kwanza hapa nchini kwa asilimia 59% .
Aidha
lengo la warsha hiyo ni kuelimisha jamii athari za ndoa Za Utotoni
hususan Mkoani Shinyanga ambapo sheria mbalimbali zimewekwa katika
kukabiliana na hilo. Bw.Golwike amesema katika utafiti mdogo uliofanywa
na Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga ulibaini kuwa 90% ya
wananchi wanafahamu kuwa ni kosa kumwozesha mtoto wa kike huku ikiamini
kuwa kumwozesha mtoto mdogo inachochea na kuvutia kupata mahari nyingi
zaidi mfano ng,ombe 25 hadi ng,ombe 50.
Hata
hivyo,Bw.Golwike amesema mradi wa kuelimisha jamii juu ya maddhara ya
ndoa za utotoni mkoani Shinyanga umefikia jumla ya watu Themanini na nne
elfu [84 ,000]kwa wilaya za Ushetu na Kishapu kati ya watu thamanini na
tano elfu [85,000]waliokusudiwa . Kwa upande wake mdau wa elimu juu ya
kupinga Mila potofu ,Paulo Robert kutoka Ukune Ushetu Mkoani Shinyanga
amesema baada ya kupata elimu naye akaitumia vyema elimu hiyo kuelimisha
watu wengine hususan Mimba na ndoa za utotoni.
Kwa
Upande wao baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria warsha hiyo wamesema
wataendelea kupambana na ndoa za utotoni katika jamii wanayoishi. Warsha
hiyo imekutanisha asasi mbalimbali za kiraia ikiwa ni pamoja na SAVE
THE CHILDREN,KIWOHEDE ,Umoja wa Ulaya,ambapo dhumuni kuu ni kuangalia
changamoto za mimba na ndoa za utotoni hususan katika mikoa 6 ya
Shinyanga,Tabora,Dodoma,Rukwa ,Manyara, na Katavi ambayo ndiyo mikoa
inayoongoza kwa mila na desturi za ndoa za utotoni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...