
Azma kuu ya Jumuiya hii si tu kukutanisha Watanzania kama sauti moja. Pia kuweka ngazi ya kusaidia , kujenga na kuwekeza nyumbani kutokea huku Majuu.
Ni jambo la kuchangamkiwa sana.
Watanzania toka sehemu mbalimbali za Uingereza walijieleza na kutafuta kura wakipigania nafasi za uenyekiti, katibu na mweka hazina na makaimu wao. Nusu ya kampeni hizi iliendelea mtndao wa WhatsApp na nusu ikakamilika ofisi za ubalozi wetu mtaa wa Bond Street, London, Jumapili 14 Julai, 2019.
Uongozi mpya wa ATUK. Waliosimama nyuma. Toka kushoto, Mweka Hazina Msaidizi, Nelson Kampa, (Birmingham); Naibu Katibu, Frank Leo (Coventry), Mweka Hazina, Lucy Shigikile (London).
Walioketi, toka kushoto,: Makamu Mwenyekiti, Zuhura Mkwawa (Leicester), Mwenyekiti , Martha Mpangile (London) na Katibu wake, Dk Imani Kondo...
Kura ikipigwa ...
Sam Mbogo mkazi Wales akijieleza kwa mintaarafu ya kupata kura
Toka kulia, Mwanahabari mkongwe na Mhariri wa The East African, Deo Kamuhanda, akiwa na Simon Mzuwanda (aliyepigania kijasiri wadhifa wa Uenyekiti na kushindwa ), Patricia Mpangala na Joe Wairoba, aliyefanya kazi kubwa kuisimamisha, ATUK.
Ukumbi umejazana Watanzania toka vitengo mbalimbali vya kisayansi, sanaa na akina mama wa TAWA.
Alex Masuguri mmmoja wa wasimamizi wakuu wa shughuli hii muhimu akitangaza matokeo. Wenzake ni kushoto, Batilda Tenga na kulia, Pauline Nzengula.
Mwenyekiti mpya, Martha Mpangile, ( pili kutoka kushoto) na Mweka Hazina , Lucy Shigikile (wa kwanza kulia ) wakipongezwa na kina mama wenzao. Picha na Habari za Freddy Macha







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...