Na Woinde shizza Michuzi Tv, Arusha.
Wazalishaji wa mbegu nchini wameanza mkakati wa kuzalisha mbegu zinazoweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ,ili kuhimili hali ya ukame na kuleta mazao mengi hivyo kumsaidia mkulima kupata uhakika wa chakula na kipato.
Akizungumza katika Maonesho ya kilimo Teknolojia yaliyofanyika katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tari Seliani ,Meneja Mauzo wa Kampuni ya Seedco Daniel Ulimboka alisema kuwa kwa sasa wamefanya utafiti na kuja na mbegu bora ambazo zinahimili hali ya ukame licha ya uhaba wa mvua bado zinaleta mavuno ya kutosha kwa mkulima.
"Tuna mbegu aina ya tumbili 419 ambayo inafanya vizuri sana hasa katika kipindi hiki ambacho hakuna mvua za kutosha wakulima bado wamekua wakipata mavuno na kufurahia kilimo" Alisema Daniel
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha aliwataka watafiti kubuni teknolojia zinazoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili wakulima waweze kupata mazao badala ya kupata hasara kutokana na mabadiliko hayo ambayo yamekua yakileta athari na kusababisha kushuka kwa uzalishaji.
Aidha aliwataka Wakulima kuondokana na kilimo cha mazoea ili waweze kufanya kilimo chenye tija na kuwaletea manufaa wakulima na taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Baraza la Nafaka Afrika Mashariki Gerald Masila alisema kuwa wanafanya juhudi za kuwaunganisha wakulima na masoko ili waweze kupata faida ya kilimo chao na kujikwamua kiuchumi.
Meneja Muzo wa kampuni ya Mbegu ya Seedco Daniel Ulimboka akifafanua juu ya mbegu za tikiti zinazozalishwa na kampuni hiyo katika maonyesho ya teknolojia za kilimo yaliyofanyika katika eneo la kituo cha Utafiti wa kilimo cha Tari Seliani na kuandaliwa na Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki.Picha na Woinde Shizza ,Arusha .
Meneja Muzo wa kampuni ya Mbegu ya Seedco Daniel Ulimboka akifafanua juu ya mbegu za tikiti zinazozalishwa na kampuni hiyo katika maonyesho za teknolojia ya kilimo yaliyofanyika katika eneo la kituo cha Utafiti wa kilimo cha Tari Seliani na kuandaliwa na Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki.Picha na Woinde Shizza ,Arusha .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...