KITUO Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kitahakikisha kinatumia kikamilifu Mkutano Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kutangaza fursa za uwekezaji zilizpo nchini hasa kwa kuzingatia soko la jumuiya hilo ni kubwa.
Akizungumza leo Julai 24 ,2019 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geofrey Mwambe amesema kuwa kituo hicho kinatambua umuhimu wa mkutano wa SADC na fursa zilizopo, hivyo wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kutangaza fursa za uwekezaji.
"SADC ni eneo kubwa la soko na Tanzania tunayo nafasi ya kulitumia vizuri.Tunafahamu tulianza na SADC iliyokuwa na lengo la kuokomboa nchi za Kusini mwa Afrika na baadae tukawa na SADC ambayo imejikita kuzungumzia maendeleo.
"Ukiitaza historia yetu, Tanzania ni mwanzilishi wa SADC iliyokuwa na CC mbili na baadae nchi zilizmo kwenye jumuiya hiyo zikaingia kwenye SADC yenye C moja.Kwetu sisi mkutano wa SADC kufanyika nchini tutatumia nafasi hiyo kujitangaza kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote,"amesema Mwambe.
Amesisitiza kupitia mkutano wa SADC unaotarajia kufanya Agosti mwaka huu wanaimini kutaibuka fursa mpya hasa kwa kuzingatia ni mkutano mkubwa na wenye kukutanisha idadi kubwa ya wananchi wa jumuiya hiyo.
Amefafanua kuwa jumuiya hiyo ya SADC ina watu milioni 450 ambalo ni soko kubwa na Tanzania inayo nafasi ya kutosha kuitumia kwa ajili ya kufanya maendeleo yake kupitia uwekezaji huku akifafanua kupitia jumuiya hiyo kuna mambo mengi ambayo nchi wanachama wamekubaliana na yanatoa nafasi kwa nchi hizo kutumia soko lililpo kufanya biashara.
Mwambe amesema kwa bahati nzuri ambayo Tanzania imepita kwani, kupitia mkutano huo Rais Dk.John Magufuli atakabidhiwa Uenyekiti wa SADC na hivyo ni fursa nzuri itakayoiwezesha nchi kutumia nafasi hiyo kujiimairisha kwenye soko la biashara kwa nchi wanachama.
Wakati huo huo Mwambe amezungmzia Kongamano la kimataifa la zao la korosho ambalo lilifanyika mkoani Mtwara ambapo amefafanua kongamano hilo limeleta tija kubwa na anaamini linakwenda kusaidia katika kuongeza thamani ya korosho nchini.
Mwambe amesema kuwa zaidi ya washiriki 400 wamahudhuria wakiwamo wageni 100 kutoka mataifa 23 duniani baada ya kongamano hilo wengi wao wameonesha nia ya kuwekeza katika zao la korosho,"amesema na kuongeza kuwa mikoa inayolima zao la korosho ya Mtwara,Lindi, Pwani na Ruvuma iko tayari kupokea wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika kuinua zao la korosho.
Ametumia nafasi hiyo kueleza umuhimu wa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya uwekezaji yawe yanaandaliwa mapema kwa kupimwa na kuwekwa michoro ili muwekezaji akipatikana iwe rahisi kuanza uwekezaji.
Kwa upande mwingine Mwambe ametoa rai kwa watanzania kuwekeza kwani wakiamua wanaweza na kikubwa ambacho wanatakiwa kukifanya ni kuunganisha nguvu ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...