*Mwito watolewa kwa wafanyabiashara kujitokeza na kutangaza bidhaa zao


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IKIWA zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa jumuiya ya maendeleo wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC) ambao utatanguliwa na wiki ya viwanda itakayoanza kesho kwa kuzinduliwa rasmi na Rais Dkt. John Joseph Magufuli katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kutengeneza masoko na kupata oda kutoka nchi 16 zinazoshiriki mkutano huo.

Akizungumza katika kilele cha siku ya wanahabari leo jijini humo Naibu Waziri wa viwanda na biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa mkutano huo ni fursa kwa watanzania hasa wafanyabiashara katika kutangaza bidhaa zao, kupata ujuzi mpya na kutafuta masoko.

"Niwaombe wananchi watumie fursa hii adhimu katika kutangaza bidhaa zao, kupokea oda, kubadilishana na kupokea ujuzi kutoka kwa wageni pamoja na kujenga ushirikiano wa hali ya juu na wageni wetu, na mmeona hata uzito uliopewa na viongozi wetu Rais Magufuli atazindua wiki ya viwanda kesho na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein atafunga wiki ya viwanda Agosti 8 hivyo tuwaunge mkono" ameeleza Mhandisi Manyanya.

Kuhusiana na idadi ya wananchi waliojiandikisha kushiriki katika maonesho hayo Mhandisi Manyanya ameeleza kuwa zaidi ya watu 2000 wamejiandikisha huku wengi wakiwa wazawa hali inayoashiria watanzania wamekubali mabadikiko na kasi ya maendeleo yanayoongozwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.

"Hadi kufikia jana idadi ya washiriki waliojiandikisha ilifikia 2000, huku wazawa wakiwa zaidi ya 700 na watakaoonesha bidhaa mbalimbali wakifikia zaidi ya 900. Kwa hali hii tunategemea matokeo chanja na maendeleo kupitia mkutano wa 39 wa SADC" Ameeleza.

Aidha Mhandisi Manyanya amewataka watanzania kuendeleza desturi ya ukarimu na uzalendo katika kipindi chote Cha mkutano ili kuweza kuendelea kupeperusha vyema bendera ya amani ya nchi yetu.

Vilevile kaimu Mkurugenzi wa mipango wa sekta ya viwanda na ushindani Dkt. barani Afrika Dkt. Johansein Rutaihwa amesema kuwa malengo ya wiki ya viwanda ni pamoja na kutoa elimu ya uelewa kuhusu mpango wa maendeleo hasa maendeleo ya viwanda uliogawanya katika vipindi vitatu ambavyo ni ule wa mwaka 2015/2020, 2021/2050 na ule 2051/2063 mikataba ambayo iliidhinishwa mwezi Machi mwaka 2015.

Amesema kuwa wiki ya viwanda imelenga kuleta ushirikiano pamoja na kutengeneza mnyororo katika ngazi mbalimbali za kitaifa na kimataifa na kubwa kuliko nikuwashirikisha wanawake na vijana katika sekta ya viwanda kwa kuwapa fursa za kuonesha gunduzi zao.

Mkutano huo wa Jumuiya ya Maendeleo wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ulifanyika nchini mwaka 2003 ambapo Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa alihudumu nafasi ya uenyekiti kwa mwaka 2003/2004 na mwaka huu Rais Magufuli atapokea kijiti hicho kutoka kwa Rais wa Namibia Hage Geingob na atahudumu nafasi ya uenyekiti kwa muhula mmoja na kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za kikanda na mikutano ya kisekta ikiwemo afya na elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...