Na Zainab Nyamka, ,Michuzi TV

Uongozi wa Klabu ya Yanga umelalamikia ubadhilifu unaofanywa na Kampuni ya Selcom Tanzania kwa kuuza tiketi mara mbili, wizi na rushwa uliotokea kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Malalamiko hayo yametolewa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredirick Mwakalebela baada ya kubaini na kuwakamata wafanyakazi wa Selcom wakiwa wanafanya wizi huo na wanajiandaa kuandika barua kwa serikali ili waweze kuchukuliwa hatua.

Kilele cha Wiki ya Mwananchi kilihitimishwa jana kwa timu ya Yanga kucheza mchezo wao wa kirafiki na Kariobang Shark’s ya Kenya na kumalizika kwa sare ya 1-1 kukiambatana na utambulisho wa kikosi kipya waliosajiliwa kwa msimu wa mwaka 209/20.

Mwakalebela amesema kuwa, wanajiandaa leo Jumatatu kuandika barua kwenda serikalini kuhusiana na utendaji wao (selcom) wa kazi mbaya ambao ulikuwa wa matukio mengi ya wizi na rushwa.

“mawakala wa kampuni hiyo walikuwa tatizo wakiwa wanauza tiketi mara mbili kwa mashabiki waliokuwa wamejitokeza na kiukweli hatukuridhishwa na utendaji kazi wao ambao kama ukiendelea, basi serikali utapoteza mapato mengi,”amesema Mwakalebela.

Ameeleza kuwa “Leo Jumatatu tunatarajia kuandika barua kwenda serikalini kwa ajili ya kuwataarifu wizi na rushwa iliyokuwa inafanyika katika kilele chetu cha Wiki ya Mwananchi, Kikubwa ni kuwafahamisha tatizo lililotokea siku hiyo ya tukio,”

Mwakalebela amesema kuwa, mbaya zaidi wameweza kukamata tiketi za Simba Day zilizopangwa kutumika kesho zimetumika kwenye tamasha letu, hivyo tunashinda kufahamu hizo pesa zinakwenda Simba au kwetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...