Na Zainab Nyamka,Michuzi TV

WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa klabu ya Simba eneo la Bunju mjini Dar es Salaam.

Uwanja huo utakaokuwa wa nyasi za bandia na nyasi za asili umewekewa jiwe la msingi na kutakuwa na kituo cha michezo, vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji na uzio wa eneo lote ambalo tayari zoezi la ujenzi limeanza.

Mwakyembe amesema kuwa Serikali inatambua uwekezaji wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohamed Dewji 'Mo' kwani waliweza kuwaruhusu waendelee na mchakato huo.

"Serikali inatambua uwepo wa uwekezaji uliopo ndani ya Simba na amekuwa bega kwa bega na viongozi hivyo nasi tunatambua uekezaji wake na wale ambao wana hofu wasiwe nayo,”amesema Mwakyembe.

Ameeleza kuwa wanaona matokeo ndani ya klabu ya Simba, wameweza kufika mbali kwenye michuano ya Kimataifa na kubwa zaidi ametoa rai kwa wanachama, mashabiki na uongozi wa Simba kuandaa ripoti ambayo itatumika kwa ajili ya kuwapa mafunzo wengine kufanya hivi kwani kila timu inapaswa ifikie hatua kubwa ambayo ni maendeleo kwenye uwekezaji wa mpira wa kisasa.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mo amesema kwamba akiwa mwanachama wa Simba na akiipenda toka utotoni ameamua kutoa fedha zake kwa ajili ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa Uwanja huo.

Mo amesema, kwakuwa ujenzi wa uwanja huo bado haujakamilika amekaa na bodi ya wakurugenzi wa Simba na wamekubali kuandaa siku maalumu ‘GALA’ Kwa ajilili ya wanachama na mashabiki 500 kuchangia fedha itakayotumika kwa ujenzi wa awamu ya pili.

Akifafanua kuhusiana na ujenzi huo, Mo amesema fedha alizozitumia kwenye ujenzi wa awamu ya kwanza hazihusiani na zile walizokubaliana kwenye uwekezaji kwenye klabu hiyo.

“Napenda kuelezea dhamira yangu kwa klabu yaSimba ni kuona inashinda kila taji inalowania katika kipindi chote, iwe na miundombinu bora na ya kisasa itakayaoiwezesha kuzalisha na wachezaji vijana watakaotokana na mipango ya muda mrefu na mfupi, kuhakikisha inakuwa na kikosi bora zaidi ya ilichonacho sasa,” amesema Mo.

Akizungumzia mipango mingine ya timu hiyo, Mo ameeleza kuwa baada ya miaka kadhaa ya kutokuwa na uwanja wetu rasmi, leo klabu hii kubwa kabisa nchini hatimaye tunatimiza ndoto zetu.

Amesema iwapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kama watakubali anataka kununua timu ya daraja la kwanza aibadilishe jina iitwe Simba B, itakayoshiriki ligi hiyo, lakini haitacheza Ligi Kuu kwa sababu hawataruhusiwa kuwa na timu mbili za ligi hiyo kubwa nchini.

Simba kesho jioni watahitimisha Simba Day kwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Power Dynamos ya Zambia na itazinduia jezi zake za msimu mpya na kutambulisha kikosi kipya kuelekea msimu huo utakaofunguliwa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akisikiliza jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji 'Mo' wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa klabu ya Simba eneo la Bunju mjini Dar es Salaam. 
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akipeana mkono na kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji 'Mo' baada ya kuweka wa jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa klabu ya Simba eneo la Bunju mjini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...