Meneja
wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania, Thobias Samwel (kulia)
akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanyika kwa droo ya
kupata washindi iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar
es Salaam. Kushoto ni Humud Semvua, mjumbe kutoka Bodi ya Taifa ya
Michezo ya Kubahatisha
Benki ya Azania (ABL) leo imewatangaza washindi wa awamu
ya
pili ya promosheni yake ya ‘Amsha Ndoto’ ambayo ina lengo la
kuwahamasisha wateja wake na umma wa watanzania kujenga utamaduni wa
kuweka akiba itakayowasaidia kuwa na maishaya baadaye yaliyo imara
kifedha.
Promosheni
hii ambayo ni ya mizezi mitatu ilianza rasmi tarehe 27/06/2019 na
inatarajia kufikiatamati tarehe 27/09/2019 huku ikihusisha wateja wa
Azania Benki wa zamani na wale wapya naimejikita zaidi katika bidhaa
mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti pamoja naWatoto
Akaunti.
Mwezi
Agosti, droo ya kwanza ya promosheni hii ilifanyika ambapo jumla ya
washindi watatuwalipatikana ambao wote kwa pamoja walijishindia jumla ya
shilingi millioni 8.Akitangaza washindi kwenye droo ya mwezi huu ambayo
imefanyika leo jijini Dar es Salaam,Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa
Benki ya Azania, Thobias Samwel, amesema benki imetimizaahadi ya
kuwapatia zawadi washindi walioshoriki kwenye promosheni na kwamba
zawadi
wanazopewa zitawasaidia kutimiza ndoto zao.
“Katika
droo iliyopita tulipata washindi kutokaArusha, Tunduma paamoja na Dar
es Salaam na wote walipewa zawadi zao kama walivyostahili,”
amesema
Samwel.Kwa mujibu wa Samwel, washindi wa mwezi huu wa promosheni hii
ambao wamepatikana baadaya droo kufanyika ni; (kiasi cha fedha
walichojishindia kwenye mabano);
1. Lucas Brian Temu kutoka Mwanza (Sh milioni 3)
2. Amos Wankara Nyansada kutoka Geita (Sh milioni 3)
3. Alye Awadhi kutoka Geita (Sh milioni 2)
Huku
ukiwa umebaki mwezi mmoja kampeni hii kufika tamati, Samwel amesema
kuwa ili mtu aweze kushiriki kwenye promosheni ya Amsha Ndoto ni lazima
kwanza awe mteja wa AzaniaBenki mwenye akiba ya kiasi kisichopungua TZS
1,000,000 ambaye anapewa tokenizinazomwezesha kufuzu kwa ajili ya droo
ya mwisho inayowapata washindi. Wanaobahatikakushinda watafurahia riba
ya 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwaka mzima.
Akitoa
pongezi kwa washindi wa promosheni, Samwel amewahasa wateja wa ABL
kushiriki kwawingi na kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi
lukuki katika droo inayofuata hukuPage 2 of 2wakijahakikishia kuwa na
akiba ya kutosha kwenye akaunti zao kwa ajili ya matumizi yao ya siku za
usoni.
Kwa
mujibu wa Samwel, ‘Ziada Akaunti’ ni kwa ajili ya watu binafsi na
wafanyabiashara wadogo (SMEs) wanaotaka kujivuna kiwango kizuri cha
riba. Mmiliki anaweza kuweka akiba muda wowote na kuweza kutoa kila
baada ya miezi mitatu. Na ‘Watoto Akaunti’ ni kwa ajili ya watoto,
akaunti ambayo inafunguliwa na mzazi kwa ajili kumwekea akiba mtoto
wake.
“Tunawahamasisha
wazazi wote na walezi kuwafungulia Watoto wao ‘Watoto Akaunti’ ili kuwa
na uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii
hawatahangaika kutafuta namna gani ya kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya
baadaye kwani akaunti hii inaweka msingi wa kuwaandaa watoto kujifunza
namna ya kuweka akiba kuanzia kwenye umri mdogo”, amesema Samwel.
Promosheni
hii, yenye kaulimbiu: ‘Weka Akiba Ushinde Tumuwezeshe Ada ya Shule’,
inawasilishwa kupitia mitandao ya kijamii na tovuti za ndani za benki.
Benki pia imetengeneza tovuti ndogo, maalumu kwa wateja wapya kujiunga
na inaweza kupatikana kupitia amshandoto.com



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...