Baaadhi ya wananchi wakiangalia gari maalum la Mahakama inayotembea mara baada ya kupaki kwenye eneo la Mahakama ya Mwanzo Buza, iliyopo Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, wakati gari hilo lilipokuwa likitoa elimu leo kuhusu Mahakama Inayotembea, ambayo imeanzishwa kwa ajili ya kusogeza huduma za Mahakama karibu na wananchi.
Karani wa Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise Mwasalemba(katikati ) akiwaelezea baadhi ya wananchi waliofika Mahakama ya Mwanzo Buza iliyopo Wilaya ya Temeke ,jijini Da res Salaam kuhusu Mahakama Inayotembea Inavyofanya wakati wa utoaji elimu kwa umma kwenye eneo hilo.
Baadhi ya viongozi wa serikali na chama cha CCM, Kata ya Buza wakipatiwa elimu leo kuhusu Mahakama Inayotembea katika eneo la Stendi ya Buza, lililopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Buza, Mhe. Florence Madelemo(katikati). (Aliyevaa shati la lightblue na mistari na kunyoosha mkono) ni Diwani wa Kata ya Buza, Mhe. James Mkude na wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Kata ya Bunza.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Buza, Shabani Abdallah akipanda katika ngazi maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wakati gari la Mahakama Inayotembea likitoa elimu kuhusu Mahakama hiyo leo kwenye eneo la Buza Stendi, lililopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Bunza, Mhe. Florence Madelemo akitoa elimu kuhusu Mahakama Inayotembea kwa wakazi wa eneo la Buza Lulenge, waliopo katika eneo la Wilaya ni Temeke jijini Dar es Salaam.
Karani wa Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise Mwasalemba(katikati ) akiwaelezea baadhi ya wananchi waliofika Mahakama ya Mwanzo Buza iliyopo Wilaya ya Temeke ,jijini Da res Salaam kuhusu Mahakama Inayotembea Inavyofanya wakati wa utoaji elimu kwa umma kwenye eneo hilo.
(Picha na Magreth Kinabo)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...