Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii

BONDIA namba moja Afrika na namba 19 duniani kwenye uzani wa super welter, Hassan Mwakinyo amejigamba kuwa fiti na hana hofu ya kuzichapa na bondia yoyote.

Mwakinyo ametoa majigambo hayo leo Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam. Kwa sasa anajiandaa kuwania ubingwa wa kimataifa  pambano la raundi 10 la uzani wa Super Welter.

"Niko fiti, yoyote atakayekuja niko tayari kuzichapa naye bila kujali anatoka nchi gani au ana uwezo gani kwenye ngumi.

"Nimelazimika kucheza pambano Dar es Salaam ili kukata kiu ya mashabiki wangu ambao tangu nitoke Uingereza nilipomchapa Samm Eggington wametamani kuniona nikicheza Dar es Salaam,"amesema Mwakinyo.

Ameongeza kuwa alipata ofa ya kucheza Kenya, lakini amekataa kwani anahitaji kucheza nyumbani ambako mashabiki wa ngumi kwa muda mrefu wametamani kumuona.
Kuhusu kucheza na mabondia maarufu nchini, Mwakinyo amesema ni suala la muda tu, kwani yuko tayari kucheza na yoyote na wakati wowote.

Hata hivyo bondia Mwakinyo kwa mara ya kwanza atapanda ulingoni kuzichapa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Oktoba 26 mwaka huu. 

Kwa upande wa Promota wa pambano hilo Jay Msangi amesema Mwakinyo atazichapa na mmoja wa mabondia kutoka kati ya nchi za Ufilipino, Italia, Marekani, Urusi au Argentina.

Ameongeza tayari amezungumza na vyama vya ngumi vya kimataifa vya WBO na IBO ili Mwakinyo agombee mkanda wa ubingwa wa vyama hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...