Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi rasmi wa Mamlaka ya hali ya hewa (TMA),  kutoka  kuwa wakala hadi kuwa mamlaka katika sherehe zilizofanyika leo Septemba 5,2019 katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Waziri wa ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akitoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa mamlaka ya Hali Hewa (TMA) kuwa mamlaka kutoka wakala kama ilivyokuwa ikitambulika mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dk.Agness Kijazi akitoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa mamlaka ya Hali Hewa (TMA) kuwa mamlaka kutoka wakala kama ilivyokuwa ikitambulika mwanza.

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

SERKALI imesema itaendelea kushirikiana na kuiwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili kufanikisha lengo la kufikia uchumi wa kati katika mwaka 2025. Pia kuyafikia malengo ya kitaifa ya maendeleo endelevu na kuakisi dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2025 na mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano.

Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamweli ameyasema hayo leo Septemba 5,2019 jijini Dar es Salaam wakati akizindua rasmi Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuwa Mamlaka kisheria kutoka kuwa Wakala. Amesema katika kuboresha huduma zake, Wakala wa Hali ya Hewa Tanzania sasa ime boreshwa na kuwa Mamlaka, lengo likiwa ni kuiwesesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na kuwa na wigo mpana kwa kuzingatia maslahi ya Tanzania Bara na. Visiwani.

Aidha amesema, Serikali katika kuendelea kuboresha huduma za TMA imekamilisha manunuzi ya rada tatu kwa kutoa fedha ili kuwa na rada saba zilizoahidiwa ambazo zitakidhi matakwa ya nchi nzima pamoja na kuwapatia eneo Dodoma kwa ajili ya kujenga Makao Makuu. Waziri Kamwelwe amefafanua kuwa lengo la Serikali ni kuwa na rada saba za hali ya hewa na kwa sasa tayari kuna rada mbili Dar es Salaam na Mwanza.Pia tayari wameanza kutoa fedha kwa ununuzi wa rada tatu zitakazofungwa Mtwara, Kigoma na Mbeya ambazo zitaiwezesha Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa ufanisi Aidha amewaahidi wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuwaangalia kwa jicho jingine ikiwa pamoja na kuangalia maslahi yao ikiwemo mishahara kwani licha ya kiwango kidogo wanachokipata sasa wamekuwa wakifaya kazi kwa ufanisi mkubwa wakati shughuli zao haziwawezeshi kufanya miradi mingine.

Katika hafla hiyo, TMA walizindua nembo mpya yenye alama ya upepo ikiwa ni chanzo cha mifumo ya hali ya hewa pamoja na mifumo mitatu ya hali ya hewa . Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk.Agness Kijazi amesema kupitia sheria mpya ya kuwa Mamlaka itakuwa imeongezea nguvu na kuratibu masuala mbalimbali ya hali ya hewa kwa lengo la kuboresha huduma zake.

Akitoa historia ya Wakala hiyo amesema ilianzishwa mwaka 1999 na kumalizika leo imekuwa na mafanikio mengi ikiwemo kuongezeka kwa kiwango cha usahihi wa utabiri wa hali ya hewa toka asilimia 75 mpaka asilimia 96 na hivyo kuifanya mamlaka kukidhi mahitaji ya sasa ya huduma za hali ya ya Hewa. Amesema mchakato wa mabadiliko ya ofisi hiyo yamefanyika chini ya sheria namba mbili ya mwaka 2019 kutoka katika wakala ambao ulianzishwa mwaka 1999.

Amesema WMO katika utaratibu wake inatambua mchango wa vituo vya hali ya hewa vya muda mrefu katika utoaji huduma hiyo ambapo mwaka huu wametambua vituo viwili nchini vya Bukoba na Songea kwa kutoa taarifa za hali ya hewa kwa usahihi kwa miaka zaidi ya 100.

"Tunalishukuru Bunge kwa uharaka wa kupitishwa kwa sheria hii imetokana na umuhimu wa shughuli za hali ya hewa nchini na kuifanya kuwa mamlaka kamili," amesema Dk.Kijazi Pia Dk. Kijazi amekabidhi vyeti viwili kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Duniani(WMO) ambayo imevitambua vituo viwili vya kusoma utabiri vya Songea na Bukoba.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mustafa Jumbe amempongeza Waziri Kamwele na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufanikisha kurejesha ndege iliyokuwa imeshikiliwa huko Afrika Kusini. Ameongeza katika uanzishwaji wa Mamlaka hiyo, Wizara yake ilishiriki kikamilifu kwa kutumia wataalamu wake kutunga sheria hiyo mpya kwa lengo la kuhakikisha TMA inatoa taarifa sahihi na zenye viwango bora kwa maendeleo ya uchumi na kijamii.

Amesisitiza wataendelea kutoa ushirikiano ili huduma zitakazotolewa ziwe na viwango bora vya kitaifa na kimataifa . Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk. Leonard Chamuriho amesema uzinduzi huo utasaidia TMA kuwa na nguvu kisheria ikiwa ni pamoja na kuongezewa nguvu ya miundombinu na rasilimali watu. Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya TMA ambae amemaliza muda wake leo Buruhan Nyenzi amesema tangu bodi hiyo kuingia madarakani mwaka 2015 wamepata mafanikio makubwa.

Ikiwemo kutunga sheria namba mbili ya Mamlaka ya hali ya hewa katika serikali ya awamu ya tano baada ya kukaa muda mrefu. Amesema sheria hiyo ndiyo ilisababisha TMA kuitwa mamlaka badala ya wakala kwani baada ya kuwa wakala walitegemea baada ya muda mfupi sheria hii itatungwa na kuwa mamlaka lakini haikuwa hivyo kwani imechukua muda mrefu mpaka mwaka huu.

Amesema, mafanikio mengine ni Tanzania kuwa nchi ya tatu Afrika katika utoaji taarifa za hali ya hewa yaani ISO 9001:2015,kuongeza usahihi wa utabiri wa msimu pamoja na vituo vya uangazi wa hali ya hewa na kuwa na mifumo mbali mbali ya usambazaji taarifa za hali ya hewa ili kuwafikia wadau kwa haraka na wingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...