KINA
mama wameshauriwa kuwanyonyesha watoto wao kuanzia umri 0 hadi miezi
sita ili waweze kupata afya bora ambayo itamsaidia kumjenga kimwili na
kiakili katika ukuaji wake.
Hayo
yalisemwa na Mratibu Lishe Mkoa wa Dar es Salaam, Neema Kweba ambapo
alisema kuwa kitendo cha kuacha kuwanyonyesha kabla ya muda kwa
kisingizio cha maziwa hayatoki kunaweza kusababisha udumavu wa mwili na
akili.
Alisema
mtoto anatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kuanzia anapozaliwa (umri
0) hadi umri wa hadi umri wa miaka miwili na zaidi huku akifikisha miezi
sita anatakiwa kupewa vyakula mchanganyiko yakiwamo maziwa ya mama
yake.
Alisema
maziwa ya mama yana virutubisho vingi ambavyo vinasaidia katika ukuaji
wake jambo ambalo linawamfanya mtoto kuwa na afya bora Na kuendelea
kukua bila ya matatizo yoyote.
"Kuna
baadhi ya kina mama wana tabia ya kuwaachisha watoto kunyonya kabla ya
wakati kwa kisingizio cha maziwa hayatoki, jambo ambalo ni uongo na
kwamba linaweza kusababisha udumavu kwa mtoto kwa kushindwa kukua
ipasavyo," alisema Kweba.
Aliongeza
kuwa, hivyo basi wanapaswa kubadilika na kunyonyesha watoto wao kuanzia
umri 0 hadi miaka miwili na kwamba wakifikisha umri wa miezi sita
wanapaswa kuwaanzishia vyakula mchanganyiko vyenye virutubisho huku
akiendelea kunyonya,hali ambayo itaimarisha afya yake.
"Ninawasihi
wanawake wenzangu acheni tabia ya kusingizia maziwa hayatoki ili muweze
kuwaachisha watoto wenu kabla ya wakati, kufanya hivyo kunaweza
kusababisha udumavu kwa mtoto au kukosa afya bora, kwa sababu maziwa ya
mama ni muhimu kwa afya yake na kwamba yanamsaidia katika ukuaji wa afya
ya mwili na akili," alisema Kweba.
Aliongeza
kuwa, mtoto anapokosa afya bora, madhara yake ni makubwa ikiwa ni
pamoja na kupata udumavu au utapiamlo, ukosefu wa kinga za mwili ,jambo
ambalo linaweza kusababisha ubongo wake kushindwa kukua ipasavyo.
Alisema
kuwa kila mzazi anayenyonyesha ana wajibu wa kuhakikisha anamnyonyesha
mtoto hadi afikie umri wa miaka miwili au zaidi huku akiendelea kumpa
chakula mchanganyiko, jambo ambalo litamsaidia mtoto kuwa na afya bora
pamoja na kumkinga na maradhi.
Alisema
mkakati wa Mkoa ni kuhakikisha kuwa wanaendelea kutoa elimu ya lishe
kwenye vituo vya afya, zahanati na hospitali pamoja na majumbani ili
kuwaelimisha wazazi au ndugu wanaobaki na watoto ili waweze kuzingatia
elimu ya lishe bora kwa mtoto.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...