Na Woinde Shizza, Michuzi TV, Arusha

Mlibwende wa dunia 2019 (miss World)Vanessa Ponce kwa kushirikiana na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian leo wametoa elimu ya hedhi salama pamoja na kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wanawake zaidi ya 100 wa shule ya sekondari ya Moshono iliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani hapa.

Vanessa ambaye ni Raia wa Mexico kwa sasa yuko mkoani Arusha,kwa ziara ya siku nne ambapo akiwa mkoani hapa amezindua mashine ya kutengeneza Taulo za kike zinazojulikana kwa jina la Uhuru Pads na kugawa taulo za kike 1000 kwa wasichana wa shule ya sekondari Moshono iliyopo katika halmashauri ya jiji la Arusha.

Akiongea wakati wa kutoa taulo hizo za kike mrembo wa dunia Sylivia Sebastian alisema kuwa amefurahi kushiriki kampeni hii ya kumsitiri mtoto wa kike ,kwani ni jambo ambalo limemgusa sana na linawaumiza watoto wengi wa kike.

"wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wanafeli masomo yao kutokana na kuwa na wasiwasi wanapokuwaga katika hedhi,wengine wamekuwa hawaji shule katika kipindi cha hedhi hivyo tumeona tuje kutoa taulo hizi za kike ili matatizo haya yanaowakumba watoto wa kike yanaisha pia tumewapa elimu kuhusiana na hedhi salama"alisema Sylivia

Akiongelea kampeni hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alishukuru mrembo huyo kwa kutembelea nchi yetu na kuipongeza kamati nzima na waandaji wa miss Tanzania kuwezesha kumleta na kuanzisha kampeni hiyo ya kugawa taulo za kike kwa wasichana wa shule za sekondari 

Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo,Dkt Harrison Mwakyembe amesema ujio wa Mrembo wa dunia(Miss World)hapa nchini katika jiji la Arusha,Venessa Ponce De Leon utasaidia kuitangaza Tanzania kibiashara ya utalii kupitia kampeni yake ya kuhamasisha matumizi ya taulo za kike kwa wanafunzi wa kike.

"pia tumpongeze Rais wetu kwa kuzia matumizi ya mifuko ya plastiki kwani zuio hilo ndio limesababisha hata wenzetu kuja na kutuletea taulo hizi za kike ambazo sio za mfuko wa plastiki kwani zinauzo na ata vifungashio vyake vinaoza na pia hata ukitupa katika choo maligafi yake inalainika na kuoza "alisema mwakimbe

Alibainisha kuwa serikali itakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha wanafanikisha kampeni hii ya kumsitiri mtoto wa kike kwakutafuta wadau ambao watanunua mashine kwa ajili yakuzalisha taulo hizo za kike ili ziweze kukithi maitaji ya watoto wakike wa sekondari zote hapa nchi . 

Naye mkurugenzi mwendeshaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi amesema hii ni mara ya kwanza kwa Mrembo anayeshikilia Taji la urembo la Dunia mwaka 2018/2019 kuitembelea Tanzania tangu kuanzishwa kwa mashindano ya miss Tanzania mwaka 1994 hapa nchini. alisema kuwa ujio wa miss dunia pamoja na muanzilishi wa shindano hili la miss World Julia Morlye ni bahati ya kipekee kwa nchi yetu ya Tanzania Kwani hii ni mara ya kwanza kwa mrembo huyu kufika hapa nchini hususa ni nchi ya Tanzania.

Alibainisha kuwa hivi karibuni mrembo wetu anatarajiwa kuondoka kuelekea nchini uingereza kwenda kushiriki shindano la mrembo wa dunia ambalo fainali yake inatarajiwa kufanyika huko hivyo watanzania wajitaidi kumpigia kura ili aweze kushinda na hata wageni hawa waendelee kuona umuhimu wa kuja nchini Tanzania huku akitaja kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka 2019 inasema urembo ni heshima hivyo kila miss Tanzania ambaye amewahi kushiriki shindano hili na anaetarajiwa kushiriki anatakiwa kutambua kauli hii na kuifanyia kazi aidha aliongeza kuwa ni jinsi gani mrembo anaweza kurudisha fadhila kwa jamii kwa kuwasaidia

kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Uhuru Sanitary pads Sara Gunda Alisema kuwa wameamua kuwapa wasichana nafasi nao wajisikie kwamba kuna watu wanawajali katika swala zima la kuvunja ungo na itambulike kuwa uwezi kuwa mwanamkekamili kama ujavunja ungo na ndio maana wakaamua kufanya hivi .

"awali kampuni yetu ilipata mthamini na kuanza kujenga mabweni kwa ajili ya wasichana na katika kutembelea mabweni yale mthamini yule aliona iko aja ya kusaidia zaidi watoto wa kike na akaona atusaidie kutengeneza taulo za kike kwa ajili ya wasichana wetu ,tulianza na kutengeneza taulo za kike zinazo fuliwa na tulivyogawa tukaona pia katika shule zetu zipo changamoto ya shule nyingi kutokuwa na maji na ndio maana tukaamua kutoa taulo hizi ambazo sio zakufuliwa ili wanafunzi wetu wasiteseke "alisema Gunda

Alibainisha kuwa hadi sasa wameshatoa taulo za kike kwa wanafunzi elfu nne waliopo katika shule za sekondari za halmashauri ya wilaya ya Arumeru ,Monduli pamoja na jiji la Arusha na hawataishia hapa bali watagawa kwa wanafunzi wa kike katika shule zote za mkoa wa Arusha , Amesema lengo ni kuendelea kutengeneza na kugawa bure taulo hizo ziweze kuwafikia wanafunzi wengi zaidi wa kike na kuondoa changamoto walionayo

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake mwanafunzi wa shule ya sekondari ya moshono Neema Msuya alishukuru kwa ujio wa miss world na kubainisha kuwa misaada waliopewa itawasaidia sana kwani kuna wanafunzi ambao wamekuwa hawaji shuleni pindi wanapokuwa katika kipindi cha hedhi kwani wengi wao wanaofia kuchafuka kitu kinachowasababishia kukosa masomo na kupelekea kufeli mitiani yao.o
 Picha ikionyesha Mlibwende wa dunia 2019 (miss World)Vanessa Ponce akiwa anatoa mafunzo ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Moshono wakati alipotembelea shuleni hapa leo na kugawa taulo za kike kwa wanafunzi hao
 mmoja wa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya moshono akiwa anauliza swala kuhusiana ya elimu waliopewa ya hedhi salama wakati miss World na miss Tanzania walienda shuleni kwao kutoa elimu
 
 mfanyakazi wa kampuni ya uhuru Amina Msuya akiwa anagawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari moshono hii leo




Muanzilishi wa shindalo la miss world Julia Morlye akiwa anaongea na wanafunzi wa shule ya sekondari moshono wakati walipotembelea shule hiyo leo kugawa zawadi za taulo za kike pamoja na kutoa elimu ya hedhi salama
 miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian akiendelea kutoa elimu ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari mushon

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...