Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi  ya SIKIKA Irenei Kiria(wa kwanza kulia) akizungumza kuhusu maandalizi ya wiki ya Azaki inayotarajia kufanyika mkoani Dodoma kuanzia Novemba nne hadi Novemba nane mwaka huu.
 Mmoja wa wadau wa asasi za kiraia akizungumza wakati wa mkutano wa Azaki na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam kuzungumzia maandalizi ya wiki ya Azaki inayotarajia kufanyika mkoani Dodoma


Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

ASASI za kiraia (Azaki) zaidi ya 500 nchini Tanzania zinatarajia kukuta katika Jiji la Dodoma kwa ajili ya maadhimisho ya wiki ya Azaki  inayoanza Novemba nne hadi Novemba nane mwaka huu.
Pia asasi hizo za kiraia zimetoa ombi kwa wadau wa maendeleo ikiwemo Serikali kujenga utamaduni wa kushirikiana kwa pamoja katika kuleta maendeleoe kwa wananchi wote nchini.

Wakizungumza jijini Dar es Salaam baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya wiki ya AZAKI wamesema pamoja na mambo mengine asasi hizo zinamchango mkubwa katika kushiriki kuleta maendeleo ingawa katika eneo hilo limekuwa na mjadala kuhusu mchango wa asasi za kiraia katika kuchangia maendeleo nchini.

Wamesema japo wakati mwingine kumekuwa kukiibuka migongano ya kimtazamo lakini lengo ni kusukuma mbele maendeleo ya Taifa na katika maendeleo kuna njia nyingi zinazofuatwa na kila moja inaweza kuwa tofauti na nyingine ingawa lengo linabaki kuwa moja tu ya kuona nchi inapiga hatua kiuchumi.

Mwakilishi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) Fulgence Massawe amesema moja ya malengo ya wiki ni kuwakutanisha pamoja wadau ikiwamo Serikali ili kuzungumza na kushuhudia shughuli zinazofanywa na Azaki katika jamii."Sisi sote tunajenga nyumba moja, hata kama inatokea tunatofautiana kimtazamo lakini lengo letu ni moja."

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi za Asasi za Kiraia Francis Kiwanga akizungumzia maadhimisho ya wiki ya AZAKI amesema wamewaalika viongozi mbalimbali wa Serikali kushiriki katika wiki hiyo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kufungua maadhimisho hayo ambayo yataanza na matembezi ya amani.

"Matembezi ya amani yatakayofanyika Jumatatu kuanzia bustani ya Nyerere Square hadi Uwanja wa Jamhuri na kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wananchi.Mbali ya Waziri Mkuu pia tumemualika Spika wa Bunge Job Ndugai, mawaziri, wabunge na viongozi wa taasisi na mashirika ya maendeleo,"amesema.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika Irenei Kiria, ameongeza kuwa kufanyika kwa wiki ya Azaki kila mwaka ni ishara kuwa kuna mambo ya msingi yanayofanywa na asasi hizo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Kiria amesema wanashukuru na kupongeza ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka serikalini ambao unafanikisha kutekelezwa kwa shughuli mbalimbali za maendeleo.

Katika  wiki ya Azaki kunatarajiwa kufanyika shughuli mbalimbali ikiwemo ya midahalo na mijadala kuhusu namna bora ya wadau wa maendeleo kwa kushirikiana na AZAKI katika kuleta maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...