Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ,Oktoba 29, 2019 wakati alipowasili nchini akitoka nchini Azerbaijan ambako alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika mkutano wa Nchi zisizofungamana na upande wowote ulifanyika jijini Baku. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, Ieo Oktoba 29, 2019 amerejea nchini akitoka Baku nchini, Azerbijan ambako alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi zisizofungamana na upande wowote.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Waziri Mkuu amepokelewa na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson Mwansasu pamoja na viongozi wengine wa Mkoa wa Dar es salaam.


Awali, Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Mataifa ya Afrika na Urusi uliofanyika katika mji wa Sochi nchini Urusi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...