Katapila likisawazisha vifusi vilivyomwagwa wakati wa ujenzi wa barabara hiyo katika kona ya Kitunda kwenda Kivule. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA
Daraja lililopo katika barabara hiyo ambalo ni takribani mwaka sasa ujenzi wake haujakamilishwa
Katapila la Kampuni ya Nyanza likiwa kazini katika daraja hilo
Kifusi kimwagwa tayari kwa ujenzi wa barabara hiyo
Kizuizi cha muda kilichichowekwa kurahisisha ujenzi
Na
Richard Mwaikenda,Ukonga.
HATIMAYE
Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza imeanza ujenzi wa Barabara ya Kitunda-Kivule,
Ukonga Dar es Salaam, baada Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutoa
amri ya kuwasweka lupango viongozi wa kampuni hiyo.
Makonda
alitoa amri hiyo Dar es Salaam Alhamisi, baada ya kampuni hiyo iliyopewa zabuni
ya kuchelewa kuanza ujenzi licha ya kulipwa malipo ya awali ya sh. bil. 4.8.
Mkataba wa ujenzi umeanza Oktoba Mosi.
Akizungumza
na vyombo vya habari, RC Makonda alisema kuwa wakandarasi hao, watakuwa akienda
kujenga barabara hiyo wakitokea mahabusu.
Pilikapilika
za ujenzi zimeanza ijumaa katika eneo la Kitunda, ambapo yalionekana makatapila
yakikwangua sehemu ya barabara hiyo, huku mengine yakisawazisha vifusi
vilivyokuwa vinamwagwa na malori.
Kampuni
hiyo itajenga kwa kiwango cha lami kipande cha barabara chenye urefu wa km 3.2
kuanzia Kituo cha Polisi Kitunda hadi Mwembeni.
Ubovu
wa barabara hiyo ya kutoka Banana, Kitunda hadi Kivule Fremu Kumi, imekuwa ni
kero na kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo. Ujenzi wa kipande hicho
cha barabara unatarajiwa kukamilika Oktoba
mwakani.
Kila msimu wa mvua kama huu barabara hiyo uharibika na kuwa na mshimo yanayosababisha daladala nyingi kusita kwenda huko, hali ambayo inawafanya abiria kulipa kiasi kikubwa cha nauli hadi sh.3000 kutoka Banana hadi Flemu Kumi kwa kutumia usafiri wa Bajaji na Bodaboda.
Wakazi wa eneo hilo wameiomba serikali kuwaonea huruma kwa kuhakikisha ujenzi wa kipande hicho kukamilika haraka kabla ya mvua za masika, lakini pia kumalizia kipande kingine cha barabara kutoka Mwmbeni hadi Flemu kumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...