Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Klabu ya Soka ya Yanga imepoteza mchezo wake wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho, hatua ya mchujo baada yakukubali kipigo cha bao 2-1 mbele ya Pyramids FC ya Misri katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Katika mchezo huo uliokuwa wa vuta mikuvute dakika zote 90, dakika ya kwanza mchezo ulianza kwa kasi zaidi kwa Yanga SC kuanza kwa spidi ya hali juu kwa kufanya mashambulizi ya hapa na pale kwenye lango la Pyramids.

Dakika ya Tisa ya mchezo, Ally Mtoni Sonso alipiga Shuti kali kwa guu la kushoto lilookolewa na Golikipa wa Pyramids, Ahmed Elshenawy kama ilivyo dakika ya 10, Kelvin Yondani kuokoa mpira kwenye chaki baada ya shambulizi golini kwa Yanga.

Dakika ya 38 ya mchezo, Beki wa Yanga SC, Ally Ally alitaka kujifunga mwenyewe  baada yakupishana na Kipa, Farouk Shikhalo kwa mpira mpira uliopigwa langoni kwao na Mchezaji wa Pyramids.

Dakika ya 42 ya mchezo huo, Pyramids FC walipata bao lililofungwa na Nyota wao, Eric Traory baada ya kupokea mpira safi ulitokea pembeni kwa lango la Yanga SC.

Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha, Pyramids walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 katika dimba la CCM Kirumba Mwanza, Yanga SC wakiwa na mashabiki lukuki zaidi ya Pyramids FC.

Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi kwa timu zote, Yanga SC walianza kulisakama lango la Pyramids, dakika ya 56, Feisal Salum (Fei Toto) anapiga Shuti kali lakini Golikipa wa Pyramids, Elshenawy anaruka juu juu nakuucheza mpira huo.

Katika kipindi hicho, Pyramids walirudi tena mchezoni dakika ya 59, Yanga SC wanapata kona dakika ya 61 lakini baada ya kona hiyo makosa ya Nyota wa Yanga, Mrisho Ngassa yanapelekea Pyramids kupata bao la pili kupitia kwa Nahodha wao, Abdallah Elsaid kuunganisha pasi safi iliyotoka kwa Mohammed Farouq.

Mshambuliaji wa Yanga SC, Juma Balinya aliingia kuongeza nguvu katika mchezo huo kuchukua nafasi ya Feisal Salum baada ya Yanga kuwa nyuma kwa jumla ya mabao 2-0, dakika ya 71 pia Mrisho Ngassa anatoka na kuingia, Deus Kaseke wakati upande wa John Antwi aliingia upande wa Pyramids kuongeza nguvu zaidi na Nahodha Abdallah Elsaid kutoka nafasi yake kuchukuliwa na Ahmed Tawfiq.

Dakika ya 88 Yanga SC walipata baokupitia kwa Nahodha Pappy Tshishimbi baada yakuwalamba chenga Beki wa Pyramids nakufunga bao hilo. Hata hivyo, Beki wa Yanga, Kelvin Yondani alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada yakucheza rafu wakati timu hiyo ikiwa na shinikizo lakusawazisha bao wakiwa nyumbani.

Kwa matokeo hayo, Yanga SC watakuwa na kibarua kizito zaidi ugenini Novemba 3, 2019 kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo nakusonga mbele, Yanga SC wanatakiwa kupata ushindi zaidi ya mabao 3-1 ili kujihakikishia nafasi ya makundi ya Michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...