Na Shushu Joel
MKUU wa wilaya ya kisarawe ambaye anakaimu Ukuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ndg. Joketi Mwegelo amewataka wananchi wa Halmashauri ya Chalinze kuwachagua viongozi wenye Utayari na Uwezo wa kuendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Bwilingu kwenye viwanja vya kituo cha mabasi Cha Barabara ya Morogoro.

Mkuu huyo wa wilaya aliwakumbusha na kuwasisitiza wananchi hao kutambua dhamani kubwa waliyonayo na yupi ni kiongozi atakayekuwa ni kiungo kikubwa kwa viongozi wa juu na anayeweza kuendana na utendaji wa Raisi Magufuli.

"Jambo hili niwewatahadharisha mapema kabla ya kufanya uchaguzi wa serikali za mtaa mwisho mwa mwezi wa kumi na moja"

Pia Mkuu wa Wilaya aliwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftali la kupiga kura huku akiwapa msisitizo kuwa ni wale watakaokuwa kwenye orodha ndani ya Daftari la Wapiga kura tu ambao watapata fursa ya kupiga kura. 

" Wananchi wenzangu wale ambao wanadhani kuwa kile kitambulisho cha kupiga kura kitawawezesha kushiriki uchaguzi huu, hapana. Uchaguzi huu tunatumia daftari hivyo ni muhimu kwenda kuniandikisha".

Alisema," jambo la kuwa na Vitambulisho kuwa kigezo si kweli bali ni wewe tu kuweza kufika kituoni na inakuchukua dakika 2 tu.

Mbali na kuwahimiza Wananchi kujitokeza katika zoezi hilo Mh.Mkuu wa Wilaya, amempongeza Mbunge wa jimbo hilo Mh.Mbunge wa Chalinze Ndg.Kikwete kwa utekelezaji na ufanikishaji wa miradi mbalimbali katika jimbo lake na juu ya yote alivyojitokeza yeye akishirikiana na wananchi kuhamasisha uandikishaji.

Hivyo amewataka wananchi hao kuwa na viongozi watakaochaguliwa vitongojini na vijijini wawe wachapakazi kama Mh. Mbunge na Mh.Raisi wanavyoshirikiana kufanya kazi nzuri ya kuleta Maendeleo." Ninyi wenyewe Mashuhuda na Mbunge ameeleza jinsi Miradi mikubwa kama ya maji,afya,madarasa, miundombinu na umeme ilivyotekelezwa kwa asilimia kubwa sana. Nakupongeza Mh. Mbunge kwa utekelezaji Mzuri wa majukumu.

Naye mzee Zaidi Lufunga (78) akizungumza kwa niaba ya Wana Chalinze amempongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kujionea mafanikio makubwa yalifanywa na serikali ya awamu ya tano katika jimbo la chalinze.

"Miaka yetu changamoto zilikuwa nyingi sana lakini kipindi hiki cha Rais Magufuli kwa kushirikiana na mbunge wetu Ridhiwani Kikwete mafanikio tunayapata na kazi nzuri inaonekana.Aidha amemwakikishia Joketi kuwa kwa hali hii ya utekelezaji wa miradi mikubwa na iliyokuwa ndio ndoto zao ni tu watachagua viongozi wenye hofu ya Mungu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete amempongeza mkuu huyo wa wilaya kwa ujio wake wa kujionea jinsi wanachalinze wanavyojitokeza katika zoezi la kujiandikisha.Amewapongeza wakazi wa kata ya Bwilingu kwa kujitokeza kwa wingi ili kumsikiliza mkuu wa wilaya. Kwake Mbunge amelielezea hili jambo kubwa na kwa hakika linatoa dalili kuwa wananchi wako tayari. 


Hadi kufikia jana Halmashauri ya Chalinze ilikuwa imefikia Asilimia 74 ya Uandikishaji na baada ya kukatika kwa mvua kumekuwa na wingi mkubwa wa wananchi kujiandikisha. Zoezi hili linatarajiwa kuisha tarehe 17 October ambapo matarajio ya kuandikisha watu 136,000 utafikiwa huku hadi jana watu zaidi ya 90,000 wakiwa wamejitokeza kujiandikisha.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...