Moureen Rogath-Buhigwe.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, amemuagiza katibu Mkuu wa wizara hiyo Leonard Akwilapo, kwenda wilayani Buhigwe mkoani Kigoma kufanya ukaguzi maalumu wa miradi ya elimu kama utekelezaji wake ulifata utaratibu.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya waziri huyo kufanya ziara katika wilaya hiyo katika miradi mbalimbali ya elimu inayotekelezwa na fedha za mpango wa lipa kwa matokeo (EP4R), miradi yenye thamani ta fedha zaidi ya Sh .1.
Waziri Ndalichako amesema katika baada ya kukagua miradi hiyo aliweza kubaini kasoro mbalimbali za ujenzi wa majengo ya elimu yanayoendelea kujengwa katika wilaya hiyo.
"Nimeweza kubaini kasoro mbalimbali katika miradi ya elimu ikiwemo matumizi ya vifaa vya ujenzi vilivyochini ya kiwango pamoja na kutumia ramani ya michoro yao binafsi na kuacha ya wizara katika majengo ya utawala", amesema Ndalichako.
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina amesema kabla ya kuja waziri aliweza kubaini baadhi ya mapungufu na kuyatolea maelekezo kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Anosta Nyamoga na kuzichukulia hatua.
"Kamati ya usalama ya wilaya iliweza kubaini mapungufu katika miradi mbalimbali na tulitoa maelekezo kupitia kwa mkurugenzi na vyombo vyetu vilishaangizwa kufanya uchunguzi na kuchukua hatua stahiki,"amesema mkuu wa wilaya hiyo Ngayalina.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo amekiri kuwepo kwa mapungufu hayo katika ujenzi wa majengo hayo ya elimu na kusema kuwa tayari ameshaanza kuchukua hatua kwa waliohusika katika ujenzi huo .
Waziri Ndalichako amekagua miradi ya elimu wilaya ya Buhigwe katika shule ya msingi Bwega , shule ya sekondari Janda, shule ya sekondari Muyama , shule ya msingi Kasumo na shule ya sekondari Mwibuye wilayani Kasulu na kubaini kasoro mbalimbali .
Waziri wa Elimu, sayansi na teknolojia akikagua ujenzi wa chuo cha ualimu Kabanga kilichopo wilayani kasulu mkoani Kigoma kinachojengwa kwa fedha za serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...