CHAMA
CHA MAPINDUZI CHAELEKEZA TBA KUKAMILISHA KWA WAKATI MAJENGO YA CHUO CHA UFUNDI
STADI KARAGWE NA KUSISITIZA KWA WADHIBITI UBORA WA ELIMU NCHINI KUHUSU UMUHIMU
WA HISTORIA YA NCHI KWA WATOTO WETU SHULENI
29
Oktoba 2019
Akiwa
katika ziara ya ukaguzi na ufuatiliaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Mwaka
2015 – 2020 Mkoani Kagera na Wilayani Karagwe Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa
Itikadi na Uenezi ameelekeza Wakala wa Nyumba wa Serikali (TBA) kukamilisha kwa
wakati Majengo ya Chuo cha Ufundi Stadi Wilaya ya Karagwe ili vijana wa
Kitanzania wanufaike na elimu ya Ufundi Stadi na kujiajiri. Ujenzi wa Majengo
mapya tisa na ukarabati wa majengo makongwe katika chuo hicho unagharimu shilingi
bilioni 4.6 ambazo zimetolewa na Serikali.
Wakati
uo huo Ndugu Polepole ametembelea na kukagua jengo jipya la Ofisi ya Udhibiti
Ubora wa elimu kwa Wilaya za Karagwe na Kyerwa ambalo ni sehemu ya Majengo 100
yaliyojengwa katika Wilaya mbalimbali nchini. Ujenzi wa jengo hilo ni sehemu ya
jitihada za Serikali ya Awamu ya tano inayoongoza na Rais John Pombe Joseph
Magufuli katika kutoa elimu bure, kuboresha miundombinu ya kufundishia, kuweka
mazingira mazuri ya kusomea, kusimamia na kuhakiki viwango vya ubora wa elimu
inayotolewa katika shule zetu za msingi na Sekondari nchini sambamba na
maelekezo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ndugu
Polepole amehitimisha ziara yake kwa kukagua utolewaji huduma katika Kituo
kipya cha Afya Kayanga na kwa kuzungumza na Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya
Karagwe ambako amewasisitiza kuendelea kujenga umoja, mshikamano na kutenda
haki katika mchakato wa Uchaguzi wa ndani ili kujiletea ushindi mnono katika
uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2019.
Imetolewa
na,
IDARA
YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA
CHA MAPINDUZI (CCM)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...