Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo  ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa  mradi mkubwa wa maji wa Kisarawe unaojengwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA.

Mradi huo ulioanza kujengwa Julai 2018 ulizinduliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu baada ya agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli kuitaka Dawasa kupeleka maji Kisarawe wakitumia mtambo wa Ruvu Juu.

Jokate amekagua mradi huo ambao umekamilika na upo katika hatua za majaribio na usawazishaji wa mandhari. 

Aidha, baada ya kujionea hatua ya mradi ilipofikia Jokate amewapongeza Dawasa kwa jitihada walizozifanya na ndani ya mwaka mmoja mradi huo kukamilika.

Wananchi wa Kisarawe wako mbioni kuondokana na adha ya ukosefu wa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa Kisarawe utakaokuwa na uwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya 20,000 mwishoni mwa mwezi huu.


Mradi huo wenye thamani ya Bilion 10.6 ukijengwa na fedha za ndani za Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) umeanza kufanyiwa majaribio Oktoba 20 ikiwa ni kwa ajili ya kusafisha tanki la maji na mabomba.

Dawasa wametumia kipindi cha mwaka mmoja kukamilisha kwa mradi huo wakifuata maagizo ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kupeleka maji Kisarawe wakitumia Mtambo wa Ruvu Juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...