Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian (kulia) akisistiza jambo wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akimkaribisha Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
Mwenyekiti na Mwendeshaji wa Shindano la Miss World Bi Julia Morley (kushoto) akisisitiza kufurahishwa kwake na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania ambapo ni mara ya kwanza kwake kuja nchini. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico (kushoto) na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian (kulia).
Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico (kushoto) na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian (kulia) wakiwa katika moja ya matukio wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian (kulia) akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico (kushoto) na Miss Tanzania 2019
Sylivia Sebastian (kulia) wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa taulo za kike
(Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
(Picha
na Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha)
Na
Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha
NI HESHIMA kubwa kwa Tanzania kutembelewa na Mwenyekiti na Mwendeshaji wa Shindano
la Miss World Bi Julia Morley pamoja na Mshindi wa Miss World 2018 Vanessa
Ponce.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa taulo za kike zinazojulikana kama Uhurupads
uliofanyika leo katika shule ya sekondari Moshono iliyopo jijini Arusha.
“Ujio wao leo hapa Arusha, ni heshima
kwa taifa. Katika mataifa yote duniani, wameichagua Tanzania, hii ni heshima
kubwa na wametuletea zawadi ya Uhurupads ambazo zitawaweka huru watoto wetu
katika kutimiza ndoto zao hasa wanapokuwa shuleni” amesema Waziri Dkt.
Mwakyembe.
Aidha,
Waziri Dkt. Mwakyembe amesema kuwa bidhaa ya taulo hizo alizozindulia leo ni
rafiki kwa mazingira kwa kuwa zinaweza kutunzwa mahali popote na zisiwe na
madhara kwenye mazingira kwa kuwa haina
mchanganyiko wowote wa plastiki. Taulo hizo zinazotengenezwa na kikundi
cha wanawake 12 kiachojulikana kama timu ya Uhuru Kit Ltd ambao wanaunga mkono
juhudi za Serikali katika kutunza mazingira kwa marufuku ya matumizi ya mifuko
ya plastiki nchini Julai, 2019.
Katika
kuhakikisha Tanzania inatumia vema fursa ya ujio wa Mshindi wa Miss World 2018
Vanessa Ponce wa Mexico, Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Serikali itaandaa ziara
maalum kwa Uongozi wa Miss World ukiongozwa na Mwenyekiti na Mwendeshaji wa
Shindano la Miss World Bi Julia Morley kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii
nchini ikiwemo mbuga za Serengeti, hifadhi ya Ngorongoro pamoja na mji wa
kihistoria wa Zanzibar.
“Uwepo wa Miss World 2018 Vanessa
Ponce, dunia nzima macho yao yapo hapa nchini, ni vema kuitangaza nchi yetu
kimataifa kupitia ujio wake” amesema Waziri Dkt. Mwakyembe.
Kwa
upande wake Mwenyekiti na Mwendeshaji wa Shindano la Miss World Bi Julia Morley
amesema kuwa amefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania
ambapo ni mara ya kwanza kwake kuja nchini.
“Nimefurahi sana Tanzania ni nchi nzuri,
nilipopanda ndege kuja hapa nilipata matangazo yanayosisitiza marufuku ya
kutumia mifuko ya plastiki, Serikali imefanya vizuri kujali kutunza mazingira”
alisema Bi Julia Morley.
Nao
Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico pamoja na Miss Tanzania 2019
Sylivia Sebastian wamesema kuwa urembo ni heshima, UhuruPads zitawasaidia
wasichana kupata elimu wakiwa huru wakizingatia kauli mbiu ya ‘Uzuri wenye
malengo.’
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na
Mwenyekiti na Mwendeshaji wa shindano la Miss World Bi Julia Morley, Mshindi wa
Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico, Mshindi wa Miss Tanzania 2019
Sylivia Sebastian Bebastian Bebwa pamoja, mwandaaji wa Mashindano ya Miss
Tanzania Bi. Basilla Mwanukuzi pamoja na walimu na wanafunzi wa shule ya
sekondari Moshono ya jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...