Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim
na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy
Myalize akizungumza na baadhi ya wateja wao wa makampuni wa jijini Mwanza,
walipokutana na kufanya mazungumzo nao wakiwafahamisha huduma mbalimbali
zitolewazo na NBC na pia kupata mrejesho kutoka kwao juu ya huduma hizo na jinsi
wanaweza kuwahudumia vizuri zaidi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo jijini humo hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim
na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy
Myalize (kushoto), akiwasikiliza wateja wa benki hiyo Malesh Mathade (kulia),
pamoja na Mitesh Metha, walipokutana na wateja wao wa makampuni mkoani Mwanza
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC
jijini humo hivi karibuni. NBC katika kipindi cha mwezi wa huduma kwa wateja
imefanya mikutano kama hiyo kwa wateja wake sehemu mbalimbali nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim
na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy
Myalize (katikati),akishikana mikono na Mteja wa NBC kutoka kampuni ya Marine
Services, Erick Hamissi, walipokutana na
wateja wao wa makampuni mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC jijini humo hivi karibuni.. Kulia ni Nelson
Julius naye kutoka Marine Services.
Meneja wa Huduma kwa Wateja Wakubwa
wa Benki ya NBC, Mary Opiyo (wa tatu kushoto), akishikana mikono na mteja wa benki
hiyo, Mkurugenzi wa Bugando Medical Centre, Padre Engelbert Nyandwi, katika
hafla waliyoiandaa kwa wateja wao wa makampuni ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa
wateja jijini humo hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni maofisa uhusiano wateja wa benki
hiyo, Abdallah Aruga na Fainess Jeremiah.
Mkuu wa Kitengo cha wafanya
biashara wa kati wa Benki ya NBC Moses Minja (kushoto), akishikana mikono na mteja
wa NBC kutoka kampuni ya Marine Services, Erick Hamissi, walipokutana na wateja
wao wa makampuni mkoani Mwanza ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wateja jijini
humo hivi karibuni. Katikati ni Mkuu wa Kitengo
cha Fedha Taslimu na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa NBC, Jimmy Myalize.
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imeendelea kuongeza na
kuimarisha huduma zake za kibenki kwa njia za kidigitali ili kuwawezesha
wafanyabiashara na wateja wengine kufanya miamala mingi ya kibenki mahali walipo imeelezwa jijini
Mwanza hivi karibuni.
Akizungumza na wateja wa benki hiyo jijini Mwanza ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC, Meneja Huduma katika Kitengo cha Wateja wa Makampuni wa benki hiyo,
Mary Opiyo alisema benki hiyo imerahisisha huduma zake nyingi kwenda kidigitali ili kuwafanya wateja wao kupata
muda zaidi wa kufanya biashara zao kuliko kupata huduma hizo katika matawi yao.
“Sasa mteja wetu anaweza kufanya malipo akiwa ofisini kwake
kwa njia ya mtandao wa intaneti akatuma pesa kwa wateja wake ambao pengine
ingebidi awapelekee au waje pale, NBC itaendelea kuboresha na pia imo mbioni kuongeza huduma nyingine bora zaidi hususan
malipo kwa njia ya mtandao ili kutengeneza fursa mbalimbali za kibiashara kwa
wateja wetu”, aliongeza meneja huyo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Kitengo cha Fedha
Taslimu na Miamala kwa wateja Wakubwa na wa Kati wa beni hiyo, Jimmy Myalize
alisema mkutano huo una lengo la kuwashukuru
wateja wao kwa biashara wanayowapa na
kuweza kuwaamini wakawa benki waitumiayo
kwa ajili ya mambo yao ya kifedha.
Alisema pia katika kukutana kwao wameweza kuwafahamisha bidhaa zao mpya, benki ipo wapi na maendeleo ya benki kwa
ujumla na pia kupata mrejesho kutoka kwao juu ya huduma za NBC na kama kuna
maeneo wangependa yaboreshwe ili kuweza kuwahudumia vizuri zaidi.
“Pia tunawakutanisha wateja wetu ili kuweza kuongea biashara
na kutengeneza fursa za kibiashara kati yao jambo
litakalosaidia wateja wetu kukua kibiashara kwani mteja anapokua na sisi kama
benki tunakua”
Benki ya NBC huadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja mwezi wa
Oktoba kila mwaka kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kutoa
misaada mbalimbali na kutoa elimu ya kifedha na ujasiriamali kwa makundi
tofauti, kutembelea wateja wao mahali walipo na
kufanya mikutano na wateja hao.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...