Na Khadija Seif, Michuzi TV
KAMPUNI ya startimes imeletea rasmi kipindi cha television chenye maudhui ya kitalii kinachotarajiwa kuruka chaneli ya ST swahili pamoja na chaneli ya Tanzania Safari.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Kampuni ya startimes David Malisa amesema, kipindi hicho kinatarajiwa kuwa na watangazaji nyota kutoka nchi ya Kenya pamoja na Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Rogers Mugisha.
"Wote wataonesha na kukueleza vivutio mbalimbali vipatikanavyo nchini Tanzania na barani Afrika ikiwemo maziwa makuu, nyota hao wataongoza katika kipindi cha Dream destination kujionea fahari ya Afrika kwa ujumla," amesema.
Pia amefafanua kuwa ndani ya kipindi cha dream destination kitaonesha wasanii wawili ebitoke pamoja na linah wakiwa katika harakati za kutembelea vivutio.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa television ya Tanzania Safari Gabriel Nderuma amesema, ni wakati wa wakuangalia maudhui yenye kujenga na kufumbua bongo za watazamaji kwa vipindi vizuri hasa vya kitalii.
"Tanzania Safari imekua ikirusha vipindi vya wanyama, maporomoko ya maji pamoja na misitu iliyopo afrika ila kwa sasa tumeweza kuongeza kipindi kingine cha dream destination kitakachoruka octoba 26 mwaka huu,"
Hata hivyo Nderuma ameeleza lengo la kuandaa vipindi vya maudhui ya utalii ni kusaidia serikali kutangaza vivutio vilivopo nchini ili kuongeza pato la taifa kwa kupitia watalii wanaokuja nchini.
Meneja wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio mpya wa kipindi cha dream destination chenye maudhui ya kitalii kinachotarajiwa kuruka katika chaneli ya ST Swahili pamoja na Tanzania Safari leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...