Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao Fc, Timu ya Yanga  imeendelea kuimarika kwa kuendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo utakaochezwa kesho Jijini Mwanza.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo Yanga wana kumbukumbu ya kuondoka na ushindi wa 2-1 kwenye Uwanja huo kwa magoli ya Heritier Makambo Amisi Tambwe.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga Hassan Bumbuli na kusema kuwa wachezaji waliokuwa timu ya Taifa, Abdulaziz Makame na Metacha Mnata pamoja na Issa Bigirimana aliyekuwa mgonjwa  tayari wamejiunga na kikosi chao Mwanza.

Kwa upande wa Kocha Zahera, amesema, baada ya mazoezi ya siku mbili vijana wake wako tayari kwa mchezo huo utakaokuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia za timu kwenye mechi zilzizopita.

"Kwa kawaida naiandaa timu kwa ajili ya mchezo uliokuwa mbele yangu, hadi sasa naona timu iko vizuri sana na iko tayari kwa mchezo dhidi ya Mbao FC. Tunawaheshimu Mbao ni timu nzuri, lakini na sisi ni wazuri pia na tumejiandaa kwa ushindi," amesema Mwinyi Zahera.

Daktari wa Timu ya Yanga, Shecky Mgazija amesema wachezaji wote wa Yanga wako kwenye hali nzuri na utimamu wa mchezo hivyo ji jukumu la kocha tu kuwatumia katika mchezo dhidi ya Mbao kesho.

Kuhusu hali ya beki wa kulia wa timu hiyo Paul Godfrey 'Boxer',  Dr. Mgazija amesema beki huyo anaendele vizuri na ataweza kuwa fiti kutumika katika mchezo dhidi ya Pyramids kama Mwalimu ataridhika na hali ya mazoezi yake.

"Kimsingi Boxer amepona, lakini hawezi kuingia moja kwa moja kikosini, hivyo anaendelea na mazoezi na ninamaamini baada ya kesho atajuika na wezake tayari kwa mchezo wa Pyramids kama atakuwa ameshaiva kwenye programu za kocha," amesema Mgazija.

Aidha amesema majeruhi mwengine Mohammed Issa Banka na Cleofas  Sospeter  bado hajajiunga na timu lakini matibabu yake yanaendelea vizuri na huenda akajiunga na wenzake baada ya timu kurejea kutoka Misri.

Wachezaji walipo kambini jijini Mwanza ni pamoja na Papy Tshishimbi, David Molinga, Deus Kaseke, Ramadhan Kabwili, Faouk Shikalo, Sadney Urikhob, Juma Balinya, Mrisho Ngassa, Ally Mtoni Sonso, Muharami Issa Marcelo, Juma Abdul, Kelvin Yondani, Feisal Salum, Ally Ally, Jafari Mohammed, Gustafa Simon, Lamine Moro, Said Juma Makapu, Raphael Daudi, Maybin Kalengo, Mapinduzi Balama, Patrick Sibomana, Mustafa Seleman na Paul Godfrey.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...