Na Woinde shizza, Simanjiro
Waziri
wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi,
mameneja wa tanesco kuwahamasisha wananchi waliopo katika Wilaya zao
kulipia umeme ili waweze kuvutiwa umeme katika kaya zote.
Aidha
alimtaka Mkandarasi ambaye ni Angelique International Ltd kwa
kushirikiana na shirika la Umeme Tanesco wilaya ya Simanjiro na mkoa wa
Manyara kwa ujumla kuhakikisha wananchi wote wilaya ya Simanjiro
katika vijiji vyote pamoja na vitongoji vyote vinapata umeme na sio
mradi Umeme tu bali ni Umeme wa uhakika.
Aliyasema
hayo jana wakati akiongea na wananchi wa Kijiji cha Naepo kilichopo
katika kata ya Naisinyai wilayani simanjiro mkoani Manyara ambapo mbali
nakuongea na wananchi hao pia alizindua mradi na kuwasha Umeme katika
Shule ya msingi Naepo pamoja na shule ya sekondari ya Shambarai zote
zipo katika Wilaya hiyo.
Kalemani
alisema kuwa anafahamu katika kijiji cha naisinyai kimeshapata Umeme
lakini haujatosheleza, lakini pia katika vijiji vingine pia vimepata
umeme ,ambapo alibainisha kuwa anafatilia katika vijiji vyote ambapo
avina umeme vinapata Umeme
"napenda
kutoa maelekezo kwa Mkandarasi pamoja na Tanesco wilaya ya simanjiro
hadi ikifika November 16 vijiji vyote pamoja na kaya zote za Kata ya
Naisinyai viwe vimepatiwa Umeme ,namaanisha kitongoji cha naepo
kiwekimejaa Umeme ,kambi ya chokaa kulipelekwa Umeme lakini bado ujaja
sasa napenda kukwambia Mkandarasi kabla ujatoka hapa hakikisha kaya
zote, vijiji vyete pamoja na kitongoji cha kibaoni kiwe kimejaa Umeme
zinaumeme"alisema Kalemani
Aliwataka
Wananchi kujitokeza kwa kasi sawa ya muheshimiwa Rais wa jamuhuri wa
muungano wa Tanzania John Magufuli kuunganisha Umeme katika nyumba zao
,alibainisha kuwa Umeme huu hautaruka Nyumba ,kitongoji, kijiji na hata
kaya na wajibu wao wananchi ni kulipia tu kiasi cha shilingi elfu 27000
na kuunganishiwa Umeme.
"napenda
kuwaambia wananchi kama nyumba yako niyamakuti ,ni tembe ama ni
yaudongo au ya gorofa zote zinastaili kuwekewewa umeme ,hakuna nyumba
isiofaa kuwekewe Umeme na olewake Mkandarasi au muhandisi au Meneja
aruke nyumba eti kwasababu ni mbaya ,hoho utakuwa wewe ni mbaya
nanapenda kukuhakikisha autabaki salama "alisema Kalemani
Mmoja
wa wananchi wa Kijiji cha Naepo Kaika Mevukori aliishukuru serikali
kwa kuwaletea umeme katika Kijiji chao Kwani umeme uwo utawasaidia
kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo Kufunga mashine za kusaga na
kukoboa, Kupungua maduka ya kuuza vifaa vya umeme pamoja na kuendeleza
shughuli mbalimbali ambazo Zilikuwa zikitegemea Umeme.
Naye
Lazaro Charles alisema wakati hakuna Umeme walikuwa wanatembea kilimeta
kumi na mbili kwenda kufata huduma za umeme kama vile kuchaji simu ,pia
walikuwa wanatembea umbali mrefu kwenda kusaga mahindi kwa ajili ya
chakula ,aidha pia alisema pia Umeme huu uliowashwa katika shule hizi
utawawezesha wanafunzi kupata muda wa ziada wa kujisomea na hata
Waalimu kupata muda wakuandaa Vipindi namitiani kwaajili ya mwanafunzi
Kwa
upande wake Laitiness Lowasa Sainyei aliomba serikali iongeze kasi
zaidi ya kusambaza umeme ili vijiji ambavyo avina viweze kupata na
wananchi waweze kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo
zinategemea umeme
Kwa
upande wake Meneja wa Tanesco wilaya ya Simanjiro, Zakaria Masatu
aliishukuru serikali kupitia Wizara ya Nishati Kwa kuendelea kuwa karibu
na Shirika katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali na hivyo
kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya maendeleo ya wananchi wa wilaya
ya simanjiro na Tanzania kwa ujumla
Alisema
kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali iliwemo udogo wa
wigo wa mradi kulinganisha na mahitaji ya wananchi, pia alibainisha kuwa
changamoto ingine inayolikabili shirika hilo wilaya ya simanjiro ni
pamoja na hujuma katika miundo mbinu hasa kuibiwa nyaya za copper kwenye
transfoma na baadhi ya Watu wasio waadilifu.
Alibanisha
kuwa wao kama shirika wanaendelea kumsimamia Mkandarasi ili kuhakikisha
anajenga miundombinu yenye ubora pia akamilishe Kazi katika muda
uliopangwa.
Waziri Wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na Wananchi Wakijiji cha Naepo kilichopo katika Kata ya Naisinyai jana mara baada ya kuzindua mradi wa umeme na kuwasha umeme katika Shule ya msingi ya Naepo iliopo katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara (picha na Woinde shizza, Manyara)
Meneja wa Tanesco wilaya ya Simanjiro Zakaria Masatu akiongea mbele ya Waziri wa nishati
Waziri Wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na Wananchi Wakijiji cha Naepo kilichopo katika Kata ya Naisinyai jana mara baada ya kuzindua mradi wa umeme na kuwasha umeme katika Shule ya msingi ya Naepo iliopo katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara (picha na Woinde shizza, Manyara) .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...