Na Woinde shizza Michuzi Tv , Arusha
Mgogoro
wa Muda mrefu uliokuwa ukifukuta baina ya familia za Marehemu bilionea
Erasto Msuya wa kugombea Mali umechukua sura mpya mara baada ya serikali
ya Mkoa kuingilia kati kwa lengo la kupata suluhu ya kudumu nje ya
Mahakama.
Mgogoro huo
ambao umedumu kwa takribani miaka 7 tangia kifo cha Marehemu mwaka 2013,
upande wa wazazi wa marehemu Erasto msuya na upande wa Mke wa marehemu
Erasto aitwaye Miriam Erasto ambaye kwa sasa yupo mahabusu Gerezani
kwa tuhuma ya mauaji ya WiFi yake,wameshindwa kuelewana juu ya
rasilimali zilizoachwa na marehemu.
Akiongea
na familia hizo katika nyumba aliyokuwa akiishi Marehemu Erasto iliyopo
Kwa Iddy wilayani Arumeru,Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro amewataka
watoto wa marehemu waliokuwa wameikimbia nyumba ya marehemu baba yao
wakihofia kuuawa kurejea katika nyumba hiyo kuanzia Leo wakati
wakiendelea na utatuzi wa mtafaruku uliopo.
Aidha
Muro amezitaka pande hizo mbili kufika ofisini kwake siku ya jumatatu
SAA 4 asubuhi wakiwa wameambatana na vielelezo mbalimbali ili kufikia
mwafaka wa mgogoro huo nje ya Mahakama.
"Si
nia ya serikali kuingilia jambo lililopo mahakamani ila kama serikali
tunamamlaka ya kusuluhisha jambo iwapo pande zote zipi tayari kuketi
kwani suala la kutafuta msindi mahakamani si suluhu ya kuleta amani"
Amesema Muro
Akiongea
mgogoro huo mtoto mkubwa wa marehemu , aitwaye Kervin Erasto alimweleza
mkuu huyo wa Wilaya kuwa wazazi wa marehemu baba yake( bibi) aitwaye
Ndeshu Msuya na babu yake aitwaye Elisaria Elia Msuya pamoja na shangazi
zake wanataka kumpokonya Mali za Marehemu baba yake .
Akijibu
tuhuma hizo,Mama wa marehemu Erasto,Ndeshu Msuya amesema kuwa wao kama
wazazi wa marehemu Erasto hawana nia ya kutaka urithi wa mali yoyote ya
marehemu mtoto wao ila wanasikia uchungu kuona Mke wa Erasto akiuza
Mali ovyo za Marehemu mtoto wao ili kumaliza suala la kesi ya mauaji
inayomhusu wakati ugawanyo wa Mali bado haujafikiwa.
Mama
huyo amedai kuhofika watoto wa marehemu kupoteza rasilimali hizo
kutokana na Mali hizo ndugu wa Mke kujimilikisha ambao wamejipa
kipaumbele kusimamia jambo ambalo linawapa mashaka kwamba huenda watoto
hao wakadhulumiwa.
Naye
baba wa marehemu aitwaye Elisaria Msuya amesema madai yanayotolewa kuwa
amejimilikisha mgodi wa marehemu Erasto hayana msingi wowote kwani
wakati anamzaa Erasto alikuwa anamiliki migodi huko Mererani na
ubilionea wa Msuya umetokana na yeye kumpa mgodi wa kuchimba madini ya
Tanzanite.
Marehemu
Erasto alifariki agosti,7mwaka 2013 kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 eneo
la Mijohoroni,wilaya ya Hai ,mkoani Kilimanjaro na watu ambao baadae
walikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela Mara baada ya Mahakama
kuwatia hatiani.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro (pili kushoto) akiwa na familia ya marehemu bilionea Erasto Msuya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...