MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu mnamo Novemba 7, mwaka huu inatarajia kutoa hukumu
dhidi ya kesi ya ya inayomkabili aliyekuwa Rais wa zamani wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake watatu.
Mbali
na Malinzi, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mtendaji wa
zamani wa Shirikisho hilo, Celestine Mwesigwa,aliyekuwa mhasibu Nsiande
Mwanga na Karani Flora Rauya.
Mapema
leo Oktoba 25, Wakili wa Serikali Ester Martin alidai Mahakani hapo
kuwa kesi hiyo ambayo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Maira
Kasonde imekuja kwa ajili ya kupangiwa tarehe ya hukumu lakini hakimu
Kasonde amepata udhuru wa kikazi hivyo Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi
amesema hukumu dhidi ya washtakiwa hao itasomwa Novemba 7, mwaka huu.
Hukumu
hiyo imepangwa kutolewa baada ya washtakiwa hao kumaliza kutoa utetezi
wao ambapo walijitetea wenyewe huku upande wa mashtaka ulikuwa na jumla
ya mashahidi 15 pamoja na vielelezo 9.
Julai 23 mwaka huu washtakiwa hao walikutwa na kesi ya kujibu aada ya mashahidi wa upande wa mashtaka kumaliza kutoa ushahidi.
Katika
kesi hiyo, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula
njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na
utakatishaji wa fedha wa dola za Marekani 173,335.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...