Na Khadija seif, Michuzi TV
MSANII wa Bongo fleva Kala Jeremiah amezindua kampeni ya kijana smart jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo Kala amesema wasanii wanatakiwa kusaidia jamii inayowazunguka kwa vitendo na kuwaandaa vijana kiakili.
Aidha, Kala ameeleza lengo la kampeni hiyo kuamsha ari, hamasa kwa vijana ili kujitambua, kutambua majukumu yao, nafasi yao uwezo na umuhimu wao katika mstakabali wa kupata jamii bora itakayoleta matokeo chanya katika mambo yote muhimu ya kijamii na kiuchumi.
"Tunaamini vijana wakijikwamua kiuchumi jamii nzima inaelewa kwa kuwa kijana ni nguzo muhimu katika jamii na taifa kwa ujumla,"
Pia amebainisha kanuni za kijana smart ni pamoja na kuhakikisha anapambana kwa nguvu na akili zake zote, kuhakikisha anapinga kwa vitendo vya mimba na ndoa za utotoni na kushiriki kikamilifu kwenye maswala ya usawa wa kijinsia pamoja na kuhakikisha anakuwa mstari wa mbele katika vita vya kupamabana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
Hata hivyo kampeni hiyo ipo chini ya shirika lisilo la kiserikali linaloitwa wana ndoto kwa kushirikiana na wadau wengine.
"Wana ndoto ni shirika changa na jipya na tutatumia njia mbalimbali ya uhamasishaji kwa vijana kupitia video kuhakikisha kijana smart imekuwa ni maisha ya kila siku ya kijana,vyombo vya habari mitandao ya kijamii vyuo na mashule nyimbo matamasha na makongamano.
Pia ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuunga mkono katika kuhakikisha vijana wanatimiza malengo yao na tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...