Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu amefungua mkutano wa Mawaziri wanaosimamia sekta za Mazingira,Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara (SADC) uliofanyika jijini Arusha.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo amezitaka nchi za Sadc kuweka mikakati na kuridhia itifaki ya mazingira ili kutunza mazingira na kuweka jitihada za pamoja za kuhifadhi mazingira ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira .

“Kazi ya Kuhifadhi na kulinda mazingira yetu ni yetu Wenyewe “ Anaeleza Makamu wa Raisi akifafanua umuhimu wa kutunza mazingira.

Makamu wa Raisi amesema kuwa serikali zinasubiri mapendekezo yanayotokana na mkutano huo kwa ajili ya utekelezaji kwa maslahi mapana ya SADC na nchi wanachama .

Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangala amesema kuwa Mawaziri hao watapitisha mapendekezo ya kuwa na mkakati wa pamoja wa kupambana na ujangili na kuhakikish kunakua na utalii endelevu.

Pia tutaangalia itifaki ya SADC Kuhusu usimamizi wa misitu ,itifaki ya mpango wa maendeleo ya utalii kwa nchi zote.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Mkutano wa pamoja wa Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC Unaojadili kuhusu mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori pamoja na Hifadhi ya Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. Mkutano huo umefunguliwa leo Oktoba 25,2019 Katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa Katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii baada ya kufungua Mkutano huo leo Oktoba 25,2019 Katika Ukumbi wa mikutano wa AICC Jijini Arusha.
Mawaziri pamoja na Washiriki wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii wa Nchi Wanachama wa SADC wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Mkutano huo leo Oktoba 25,2019 Katika Ukumbi wa mikutano AICC Jijini Arusha .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...