Mvua zinazoendelea kunyesha mkoa wa Tanga zimezidi kuleta maafa, baada ya usiku wa kuamkia leo Oktoba 26, 2019 kukata barabara kati ya Handeni na Korogwe katikati ya kijiji cha  Misima na Sindeni. Pichani ni gari la abiria aina ya Noah likiwa limetumbukia mtoni. Noah hiyo inayodaiwa ni ya abiria, na ilikuwa inatoka Handeni kwenda Korogwe, ilipofika hapo alfajiri ya leo, dereva hakujua kuwa barabara imekatika, hivyo akajikuta anaingia kwenye mto. Inadaiwa watu kadhaa wamepoteza maisha.

Kwa taarifa iliyotufikia kwenye chumba cha habari inaelezwa kuwa watu nane wanadaiwa kufariki baada ya gari walilokuwa  wakisafiria aina ya NOAH kutumbukia mtoni kutokana na Daraja kukatika Wilayani Handeni mkoani Tanga.Habari zaidi tunafuatilia kwa Mamlaka husika. 

Wasafiri kutoka Dar es Salaam na mikoa mingine wamekwama katika eneo la Mandela kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara katikati ya wilaya ya Handeni na Korogwe, Mkoani Tanga baada ya kufurika kwa mto Mandera kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa nchini.  Hii ni mara ya pili sasa kukatika kwa mawasiliano katika eneo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...