Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kuitendea haki kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Mhasibu Mkuu wa zamani Takukuru, Godfrey Gugai na wenzake watatu kwa kuwa mashtaka yanayowakabili watuhumiwa hao hayana dhamana.
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ameeleza hayo leo Oktoba 21, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini upande wa mashtaka kupitia wakili wa Serikali Silivia Mitanto kudai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini mawakili wanaosimamia kesi hiyo hawapo wapo mahakama ya mafisadi.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba alisema hajafurahi kuona kesi hiyo inaahirishwa kwani lazima waitendee haki kwa sababu mashtaka yanayowakabili washtakiwa hayana dhamana.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 28 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.
Mbali na Gugai, washitakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga na Leonard.
Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake wawili, wanakabiliwa na mashtaka 40, kati ya hayo, makosa 20 ni ya utakatishaji fedha na 19 ya kughushi.
Kwenye mashtaka hayo 29 yanamkabili Gugai peke yake ikiwemo ya kumiliki mali zilizozidi kipato halali yenye thamani ya Sh.Bilioni 3.6 inadaiwa alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decembeaahirishwa 2015.
Pia Gugai na Makaranga wanashtakiwa kutakatisha fedha. Aidha Gugai na Aloys wanakabiliwa na mashtaka manane ikiwamo manne ya kughushi na manne ya utakatishaji fedha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...