Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MATAIFA 16 Barani Afrika  yamefanikiwa kutinga Fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) 2020 nchini Cameroon.

Mechi za mwisho zilipigwa siku ya Jumapili na kwa timu 16 kukamilika, huku vigogo wa soka Wakitupwa nje ya fainali hizo.Timu ya Ghana 'Black Stars' imeshindwa kuifunga timu ya Burkina Faso katika  mji wa Ouagadougou.

Senegal, pia ni timu kubwa iliyoondolewa katika fainali hizo baada ya kushindwa na Guinea kupitia mikwaju ya penati.Senegal ilienda Conakry ikiwa kifua mbele kwa bao 1-0 lakini Guinea ilijitutumua katika mechi yao ya nyumbani na kujipatia ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mamadouba Bangoura.

Baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi zote, wenyeji walifuzu kupitia mikwaju ya penalti 3-1.Ivory Coast ilishindwa kufuzu katika fainali hizo licha ya kushinda mechi yao ya nyumbani dhidi ya Niger 1-0.

Timu hiyo ilishindwa mabao 2-0 na Niger katika mkondo wa kwanza na kuondolewa kupitia wingi wa mabao 2-1 .Tanzania ilikuwa ni nchi ya pili kufuzu fainali hizo baada ya kuwaondoa Sudan kwa wingi wa mabao  baada ya kutoka sare ya 2-2.

Zimbabwe imejitakatia tiketi ya kushiriki mashindano hayo ya Cameroon mwaka 2020 baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Lesotho lakini ikafuzu kwa wingi wa mabao 3-1.DR Congo iliichapa Jamhuri ya Afrika ya Kati mabao 4-1 mjini Kinshasa ushindi ambao uliwapatia jumla ya mabao 6-1 huku nao Congo Brazzaville wakifuzu kwa bao 1-0 la nyumbani dhidi ya Equatorial Guinea na kunyakua jumla ya mabao 3-2.

Katika eneo la kaskazini,Tunisia ilijikatia tiketi ya mashindano hayo baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 3-1 dhidi ya Libya.
Mali pia itashiriki mashindano hayo baada ya Cameroon, baada ya kuinyuka Mauritania jumla ya mabao2-0.

Nigeria iliathiriwa zaidi katika mashindano hayo baada ya kushindwa na Togo siku ya Jumamosi huku bingwa watetezi Morocco wakipata ushindi dhidi ya Algeria.

Timu zilizofuzu kwa mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, (CHAN) yatakayoandaliwa na Cameroon:

Cameroon (mwenyeji)
Tanzania
Uganda
Rwanda
Zambia
Namibia
Togo
Morocco
Zimbabwe
DR Congo
Congo
Tunisia
Burkina Faso
Guinea
Niger
Mali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...