Mkuu wa eneo la maandalio la kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayoyosi ya Mufindi Mchungaji Dkt Antony Kipangula (wa pili kushoto ) akiwa ameshikana mikono na wachungaji na viongozi wa dayosisi hiyo jana kuonyesha umoja wakati wakizungumza na waandishi wa habari juu ya kutengwa kwao na dayosisi ya kusin
Mhubiri wa kimataifa kutoka Israel,Rabbi Abshalom akihubiri katika mkutano wa injili kijiji cha Ikongosi Mufindi ulioandaliwa na kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzani (KKKT)eneo la maandalio ya dayosisi ya Mufindi juna (PICHA NA FRANCIS GODWIN)
Wachungaji na viongozi wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) eneo la maandalio ya dayosisi ya Mufindi wakiwa katika mkutano wa injili kijiji cha Ikongosi wakimsikiliza mhubiri wa kimataifa kutoka Israel ,Rabbi Abshalom(hayupo pichani) jana
………………..
NA Francis Godwin , Iringa
MKUU wa eneo la maandalio la kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Mufindi mkoani Iringa Mchungaji Dkt Antony Kipangula amewataka wakristo kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali ya mitaa na uchaguzi mkuu mwakani ili kupata viongozi wenye sifa za kizalendo watakaofanya kazi na Dkt John Magufuli ya kuwaletea maendeleo watanzania pasipo ubinafsi na kuendekeza migogoro.
Akizungumza jana wakati wa kilele cha mkutano mkubwa wa injili ulifanyika katika kijiji cha Ikongosi chini ya mhubiri wa kimataifa Rabbi Abshalom kutoka Israel , jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli zinaliletea heshima kubwa Taifa na kila mtanzania anaona kasi kubwa ya maendeleo ambayo imekuwa ikifanywa na serikali katika kuliwezesha Taifa kujitegemea pasipo kutegemea wahisani .
Hivyo alisema mwendo huo ambao Rais Dkt Magufuli amekuwa akiendanao katika kuliwezesha Taifa kupiga hatua ni vema watanzaia kama walivyojitokeza kwa wingi kujiandikisha na viongozi wa dini kama walivyohamasisha waumini wao kujiandikisha ndivyo wanapaswa kufanya uhamasishaji mkubwa wa watu kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali na siku ya kupiga kura kila mmoja kufika kituoni kuchagua kiongozi mwenye sifa ya Rais Dkt Magufuli ya kuwatumikia wananchi na wale wasio na sifa wasiwapigie kura .
“ Eneo la dayosisi yetu ya maandalio dayosisi ya Mufindi tumejiwekea mkakati wa kila jumapili tunapokutana katika ibada zetu kuwa na kipengele cha kuwaombea viongozi wetu akiwemo Rais ,makamu wa Rais waziri mkuu ,mawaziri ,wakuu wa mikoa na wilaya na hadi viongozi wa ngazi za vitongoji lengo la kufanya hivyo ni kumwomba Mungu awaongoze katika utendaji kazi wao wa kila siku na wasijikwae katika kuwatumikia watanzania na tumekuwa tukiona unyofu nauadilifu wa Rais wetu katika kuwatumikia watanzania “ alisema Dkt Kipangula
Kuwa hakuna mtu ambae ambae haoni kazi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt Magufuli kwenye utawala wake miradi mikubwa ya kimaendeleo imefanyika kwa miaka hii mitano kwa kuwa na ndege za kutosha ,reli imeimarishwa , mradi mkubwa wa umeme Rufiji , miundo mbinu ,afya ,elimu bila malipo na mambo mengi makubwa ambayo yote hayo yanafanyika kutokana na uzalendo mkubwa kwa Taifa ambao Rais ameonyesha .
Alisema pamoja na kuendelea kuliombea Taifa kuzidi kuwa na mshikamano na umoja bado jukumu la kila mtanzania kuendelea kumuombea Rais afya njema na wale wasiolitakia mema Taifa kwa kutoa maneno yasiyo faa kwa serikali na Rais kuombewa ili roho mbaya kwa Taifa zisiweze kujiinua .
Mchungaji Dkt Kipangula alisema watu wenye roho mbaya sasa wameanza kuingia hadi kwenye nyumba za ibada kwa kutengeneza migogolo na chuki jambo mbalo ni hatari na serikali haina budi kuingilia kati kwa kuchukua hatua za haraka pale penye chuki na migogolo maana migogolo ndani ya nyumba za ibada ni mibaya zaidi na inajenga chuki mbaya zaidi na kama amani haitakuwepo kwenye nyumba za ibada ni vigumu Taifa kuwa na amani .
“ Mfano KKKT dayosisi ya Kusini kwa sasa ipo kwenye mgogolo na jimbo la Mufindi ambalo sasa ni eneo la maandalio ya dayosisi ya Mufindi toka mwaka 2015 ilipotengwa na uongozi wa juu ya dayosisi ya kusini ila kwa kuwa tunamwamini Mungu sisi Mufindi tumesimamia imara na kuupa kisogo mgogolo huo pamoja na kutengwa kwetu sisi kazi ya Mungu inasonga mbele tena kwa kufanya mambo makubwa zaidi kufanya kazi ya kitume tuliyotumwa kuifanya na kuhubiri injili isonge mbele “
Aidha alisema jukumu la kuliombea Taifa na viongozi wake ni la dini zote na kila mtanzania anawajibu wa kumuombea Rais na serikali pia kila mmoja ana nafas ya kukemea wale wanaovuruga amani ndani ya nyumba za ibada na nje ya nyumba za ibada maana nchi hii ni moja amani ikivurugika wote tutaangamia .
Kwa upande wake mchungaji mstaafu wa KKKT Antony Mabena alisema kuwa kutengwa kwa waumini wa jimbo la Mufindi na dayosisi ya kusini kwao si hoja kubwa ya kushindwa kumwabudu Mungu na kuwa kwa kuwa wanamwamini Mungu si mwanadamu mambo yote ya ibada na maendeleo ya eneo hilo la maandalio ya dayosisi ya Mufindi yanakwenda vizuri .
Alisema Mungu si wa machafuko wala chuki bali ni Mungu wa upendo na mshikamano na kutengwa na mwanadamu si tija kwani Mungu ni wa upendo hivyo wamesimama kidete kwa kuwa wanajua wanayemtegemea si mwanadamu ni Mungu .
Martine Ngwembe mwenyekiti wa mchakato wa jimbo la Mufindi kuelekea kuwa dayosisi ya Mufindi kuwa wanaamini kabisa kupiga hatua mbele kwa kumtanguliza Mungu na tayari hata kama bado mkuu wa KKKT hajabariki rasmi Mufindi kuwa dayosisi ila kazi zinazofanyika kwa kimaendeleo ni kubwa na zinazidi hata zile za dayosisi yenyewe na kuwa wao lengo ni kusonga mbele na hawataangalia nyuma wasije wakageuka jiwe la chumvi.
Alisema kuna hoja ya askofu mstaafu wa dayosisi hiyo Isaya Mengele kuwa kuna wachungaji 18 ambao amewakabidhi kwa askofu mpya kuwa hoja hiyo haina ukweli kwani wachungaji 18 anaosema ni wale alioagiza polisi wakamatwe na kuwekwamahabusu Octoba 6 mwaka 2015 kituo cha polisi cha Mdandu ambao bado wako huko kwani hakuna aliyekwenda kuwatoa .
Hivyo alisema hakuna sababu ya kuwatambua wachungaji hao wakati hakuna kiongozi aliyekwenda kuwatoa polisi wala kuwa na mawasiliano na jimbo la Mufndi hadi leo na mkutano mkuu huo wenye maamuzi ya juu jimbo la Mufindi halikushirikishwa na hadi leo hakuna ushirikiano wowote hivyo ndio maana wapo kwenye eneo la maandalio ya dayosisi yao ya Mufindi chini ya uangalizi wa askofu wa mstaafu wa dayoyosi ya Iringa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...