Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuuawa kwa kiongozi mkimbizi wa wapiganaji wa Islamic State (IS) kaskazini magharibi mwa Syria.
Akizungumza kutoka Ikulu ya White House, bwana Trump amesema Abu Bakr al-Baghdadi alijilipua wakati alipozingirwa na kikosi maalum cha Marekani.
Katika hutuba isioyakawida siku ya Jumapili , Rais Trump alisema Baghdadi alikufa baada ya ya kufika ukingoni alipokuwa akitoroka huko "akilia na kupiga mayowe wakati anafukuzwa na mbwa wa Marekani".
Baghdadi wakati huo alikuwa anatoroka akiandamana na watoto wake watatu wadogo ,lakini hatimae akajilipua kwa bomu alilokuwa amevaa baada ya kugundua kuwa amezingirwa.
Katika mlipuko huo Baghdadi na hao watoto wake wote watatu walifariki papohapo.Rais Trump alisema japo mwili wa Baghdadi ulikuwa umechanika lakini waliweza kumtambua baada ya kuufanyia uchunguzi.
"Jambazi ambae alijitahidi sana kuwaogofya na kuwahangaisha wengine siku zake za mwisho alionekana mwenye mahangaiko ,taharuki kubwa na kuchanganyikiwa ,alionekana mwenye uoga kupindukia alipogundua kikosi cha Marekani kilikuwa kinamkaribia , Rais Trump alisema.
Baghdadi alipata umaarufu mwaka 2014, alipotangaza kubuniwa kwa "himaya ya Kiislamu" katika maeoneo Iraq na Syria.Wapiganaji hao walianzisha utawala wa kikatili dhidi ya watu wapatao milioni nane katika maeneo waliokuwa wanayashikilia.
Kundi hilo pia linalaumiwa kwa kufanya mashambulizi kadhaa katika miji mbalimabli duniani.Kundi hilo la IS linalaumiwa kwa udhalimu pamoja na maovu yaliyosababisha vifo vya maelefu ya watu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...