Na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri ameahidi kumsaidia fedha shilingi milioni moja mtuhumiwa sugu aliyekili na kuhusika kwenye makosa mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi,baada ya kujisalimisha mbele ya Kamati ya ulinzi na Usalama ya Manispaa hiyo.
Kauli hiyo ameitoa leo mbele ya waandishi wa habari na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Manipsaa hiyo mara baada ya Ali Mtemi ambaye ni mtuhmiwa sugu wa uhalifu kufika na familia yake mbele ya kamati hiyo na kukili kuhusika kwa baadhi ya matukio huku akitubu na kuomba msamaha kwa kujutia kile alichokifanya kwa muda wote.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (kulia) akizungumza mbele ya waandishi wa habari, ambapo ameahidi kumsaidia fedha shilingi milioni moja mtuhumiwa sugu aliyekili na kuhusika kwenye makosa mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi ambapo amejisalimisha mbele ya Kamati ya ulinzi na Usalama ya Manispaa hiyo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akimpongeza mtuhumiwa sugu aliyekili na kuhusika kwenye makosa mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi ambapo amejisalimisha mbele ya Kamati ya ulinzi na Usalama ya Manispaa hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiwapongeza ndugu wa mtuhumiwa sugu aliyekili na kuhusika kwenye makosa mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi ambapo amejisalimisha mbele ya Kamati ya ulinzi na Usalama ya Manispaa hiyo.kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,Ng’wilabuzu Ludigija.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...