25 Oktoba, 2019.
Ndege mpya ya pili aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na
Serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeondoka nchini
Marekani kuja Dar es Salaam Tanzania.
Ndege hiyo kubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 inatarajiwa kutua
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es
Salaam leo mchana Oktoba 26, 2019.
Ndege hiyo itapokelewa na wananchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Hii inakuwa ndege ya 8 kati ya ndege 11 zilizonunuliwa na Serikali kwa
lengo la kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kukuza utalii na
uchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...