Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu amepongeza mafunzo ya ndani yaliyokuwa yanatolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo juu ya Sheria ya Ununuzi wa Umma pamoja na kanuni zake.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo, Dkt. Bujulu amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa VETA kutokana na Mamlaka hiyo kuwa na udhaifu na mapungufu katika Manunuzi.

Dkt. Bujulu amesema PSPTB imefanya jambo muhimu kutoa mafunzo hayo, amesema suala la manunuzi linajumuisha Idara mbalimbali, amesema VETA imevunja miradi yake mingi, mikataba kutokana na upungufu wa Manunuzi.

"Niseme tu, Mafunzo haya ya siku mbili hayatoshi, huenda tukaitisha mafunzo tena ili tuelewe vizuri zaidi kuhusu masuala ya Ununuzi na Ugavi katika idara zetu za VETA", amesema Dkt. Bujulu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye amesema mafunzo hayo yamelenga Watumishi wa VETA walikuwa Makao Makuu kwenye maeneo yanayohusiana na utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma.

Bilabaye amesema mafunzo hayo yamehusu zaidi maeneo yanayoweza kuboresha utekelezaji na usimamizi wa miradi kutumia miongozo, kanuni na sheria ya Umma.
 

Mafunzo hayo yalikuwa na Malengo yafuatayo:-

1. Kujenga uelewa wa pamoja kati ya wadau wa ndani (Idara tumizi, kamati za tathimini na Bodi ya Zabuni) juu ya taratibu za kuzingatia katika kutekeleza miradi na shughuli mbalimbali kwa ufanisi

2.Kutatua changamoto zilizopo ili kuongeza tija na kupata thamani ya fedha katika ununuzi wa bidhaa, huduma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa VETA Makao mkuu mara baada ya kumalizika kwa mafunzo yaliyofanyika siku mbili kuanzia Oktoba 25 hadi 26, 2019 katika ukumbi wa ofisi za VETA Makao Makuu, Chang`ombe jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye akizungumza jambo wakati wamafunzo kwa Wafanyakazi wa VETA yaliolenga kujenga uelewa wa pamoja kati ya wadau wa ndani ya Mamlaka hiyo (Idara tumizi, kamati za tathmini na Bodi ya Zabuni) juu ya taratibu za kuzingatia katika kutekeleza miradi na shughuli mbalimbali za ununuzi kwa ufanisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa wafanyakazi wa VETA yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) pamoja na VETA Makao Makuu yaliyofanyika katika ukumbi wa VETA Makao Mkuu, Chang`ombe jijini Dar es Salaam leo.

Mshauri wa masuala ya Ununuzi na ugavi, Hamis Mpinda akitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa VETA yaliyokuwa yanahusu sheria ya Ununuzi wa Umma pamoja na kanuni zake yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 25 hadi 26, 2019 katika ukumbi wa ofisi za VETA Makao Makuu, Chang`ombe jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye akichangia mada wakati wa mafunzo kwa Wafanyakazi wa VETA ambayo pia yalilenga kutatua changamoto katika ununuzi ili kuongeza tija.

Baadhi ya Wafanyakazi wa VETA Makao makuu wakichangia mada wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na PSPTB pamoja na VETA Makao yalikuwa yanahusu sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 25 hadi 26, 2019 katika ukumbi wa ofisi za VETA Makao Makuu, Chang`ombe jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa VETA Makao makuu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa na PSPTB pamoja na VETA Makao yalikuwa yanahusu sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 25 hadi 26, 2019 katika ukumbi wa ofisi za VETA Makao Makuu, Chang`ombe jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...