Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Serikali imesema kuwa Wananchi wawe wanachukua tahadhari katika kipindi cha mvua wakati wanatumia vyombo vya usafiri.

Hayo ameyasema Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi  Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe  wakati akizungumza na waandishi habari leo kuhusiana kukatika kwa mawasiliano katika Barabara mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Tanga.

Amesema kufuatia kwa mvua hizo wamesitisha safari za train ya mizigo kwa Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro.

Kamwelwe amesema kuwa mvua zilizonyesha kwa Mkoa wa Tanga ,miundombinu ya Barabara imekuwa na changamoto na kufanya serikali na vyombo vyake kuweka kambi.

Aidha amesema kuwa mvua zikiisha tu watajenga kwa haraka kwani fedha zipo za kufanya ujenzi huo.

Amesema Tanga imeaathiriwa sana katika miundombinu ya Barabara   na hizipitiki katika Wilaya za Handeni,Korogwe,Pangani,Mheza Pamoja na Lushoto.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hatua iliyochukua kufuatia na Mvua ilyoharibu miundombinu ya Barabara katika Mkoa wa Tanga leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...