
Na.Vero Ignatus Arusha.
Wizara ya maliasili na utalii imepiga marufuku wananchi kuuza nyama pori wakati ikiendelea na kupitia kanuni na rasimu,ambapo ifikapo desemba mwaka 2019, kanuni hizo zitakuwa zimekamilika na watatangaza kwa umma ,maeneo yatakapokuwepo mabucha hayo ,na serikali itaendelea kudhibiti biashara hiyo ,ili mwananchi aweze kununua nyama hiyo kwa njia halali.
“Haitachukua muda mrefu kanuni hizi zitatoka na tutatoa maelekezo watu wanaotaka kufungua hayo mabucha watayafungua kwa utaratibu gani”
Hayo yamekuja baada ya Mhe.Rais Magufuli akiwa mkoani Katavi alitoa maagizo kwa Wizara hiyo, huku akikumbushia maagizo ambayo alikwisha yatoa kwamba, ihakikishe inaanzisha mabucha ya kuuza nyama pori ili kuondoa na kudhibiti vitendo vya ujangili na kuwapa fursa wananchi waishi pembezoni mwa hifadhi kupata kitoweo kwa kuwa ni chakula chao cha asili.
Akizungumza jana Jijini Arusha na vyombo vya habari Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolfu Mkenda alisema kuwa wizara itaendelea kudhibiti na kuhakikisha hakuna mwananchi hata mmoja atakayeruhusiwa kuuza nyama pori hadi pale serikali itakaporidhia.
“Sasa hivi tunapambana sana na ujangili wawanyama pori ambao wanakamatwa kwa mitego kaskazini mwa Serengeti,imeanza kuingia kidogo maeneo ya seluu,tunakamata watu sana lakini baadhi ya wenyeji wa kule nyama pori ni chakula chao cha asili”Alisema Profesa Mkenda.
Alisema kuwa wanyama wote watakaowindwa kwaajili ya kuuzwa kwenye mabucha lazima wapimwe na waganga/Madaktari kwasababu wanyamapori wanamagonjwa mengi ambayo yamnaweza kuleta athari kwa afya ya binadamu.
“Wanyama pori wana magonjwa kuliko mifugio ya kawaida ni lazima wapimwe,wajulikane wajulikane wale wanaotakiwa kitaalamu kwaajili ya kuliwa ili kuondoa changamoto ya wananchi kupata maradhi yatokanayo na wanyama pori.Alisema Profesa Mkenda.
Agizo hilo limekuja baada ya waandishi wa habari kutaka kujua mchakato wa uanzishaji wa mabucha ya nyama pori utaanza lini na vilevile wizara imejipangaje kuhakikisha zoezi hilo linaepuka ujangili wawanyama.
Profesa Mkenda akijibu maswali hayo amesema kuwa Wizara lazima ipitie Kanuni na rasimu kwani tayari imekamilika vizuri na imeshawasilishwa kwa Waziri,zitajadiliwa,zikishapita zitatolewa rasmi kama kanuni,kisha waanze kufungua mabucha, ili wananchi wanaoishi kando ya hifadhi waweze kupata fursa ya kupata kitoweo hicho kwa bei inayoendana na hali zao kama yalivyo maagizo ya Mhe.Rais.
Ametanabaisha kuwa baada ya kupitishwa na waziri hiyo itakuwa fursa ya kununua nyama pori ndiyo maana hadi sasa wamekuwa wakipeleka maeneo mbalimbali yakiwemo kwenye matamasha ya urithi wetu na wamekuwa wakitoa bure kwasababu hakuna kanuni ya uuuzwaji wa nyama pori.
Alisema wananchi ambao wananishi pembezoni mwa hifadhi ambapo nyama pori ni chakula chao cha asili ,hivyo watahakikisha kuwa kunakuwepo na usawa wa bei ambayo mtu atanunua kwa njia halali,zisijeuzwa mijini mijini peke yake.
Pia alisema kanuni hiyo itatoa mwongozo aina ya wanyama watakaowindwa ,bei na utaratibu mzima wa uwindaji wao na namna ya kufungua mabucha hayo kwa haraka zaidi kwa manufaa ya watanzania kwa ujumla.
“Mfano mnyama mbogo anatembea na magojwa ambayo yanaweza kumuathiri binadamu ,Yule atakayeruhusiwa kuuza nyama piori lazima apate kibali cha wagani ,hatuwindi wanyama majike,watoto bali wale wqanaokubalika kitaalamu, yanaweza kumwambukiza hatutakuruhu nyama pori kiholela tutakukamata .Alisema Profesa Mkenda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...