Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa elimu ya Kichwa na Mgongo Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga leo kulia ni Mjumbe wa Chama hicho Taifa Oscar Changala
 OFISA Habari wa Mkoa wa Tanga Zuberi akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 SEHEMU ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania 
 MWENYEKITI wa Klabu ya Waaandishi wa Habari Mkoani Tanga Hassan Hashim akichangia jambo kwenye mkutano huo
Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima Mkoani Tanga Mbaruku Yusuph akiuliza swali kwenye mkutano huo.

WAGANGA wa Kinyeji hapa nchini wametakiwa kuacha kuwapokea na kuwapa tiba watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi badala yake wawahimiza wazazi kuwapeleka hospitalini kupatiwa matibabu ili kuondosha tatizo hilo.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa elimu ya Kichwa na Mgongo Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

Alisema kwani kumezuka tabia ya baadhi ya waganga wa kienyeji kuwapokea wagonjwa hao huku wakijua kwamba hawawezi kuwatibia matatizo waliokuwa nayo jambo ambalo limepelekea asilimia kubwa wengi wao kuzidiwa na ugonjwa walinao.

“Ndugu zangu waganga wa kienyeji achani kuwapokea na kuwapa tiba watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi badala yake wazazi wahakikishe mnawapaleka kuwapeleka hospitalini kupatiwa matibabu ili kuondosha tatizo hilo”Alisema.

“Lakini pia acheni kusema kwamba watoto wenu wamerogwa, balaa wala mikosi bali wapelekeni hospitalini wapate tiba ya magonjwa yanayowakabili “Alisema

Hata hivyo aliwataka pia wasiende kwenye maombi,makanisani wale misikitini badala yake waende hospitalini kwenda kupatiwa matibabu ambayo yatawasaidia kuondokana na matatizo yanayowakabili.

“Wananchi achaneni na imani potofu juu ya ugonjwa huo huku akitaka waupige vita kwani baadhi yao wana imani kuwa ni mizimu jambo ambalo halina ukweli wowote.

Awali akizungumza katika mkutano huo Afisa Ustawi wa Jamii Mmasa Malugu aliwataka waandishi wa habari kutumia vema kalamu zao ili kuweza kusaidia kuwafichukua watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi waliopo kwenye jamii.

Alisema kwamba lazima jamii ibadilike na kuondokana na fikra potovu kuhusiana na kuwaficha watoto wenye matatizo hayo badala yake wawapeleke hospitali ili waweze kupatiwa matibabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...