Startimes wanakuletea Tamthilia nzuri ambayo itavutia macho ya watazamaji wengi iitwayo THE LOST HEARTS, itaanza kurushwa siku ya Jumapili tarehe 27 mwezi oktoba  kwenye chaneli ya ST Novela Eplus saa 3:45 Usiku. Tamthilia hii itakuja baada ya Tamthilia ya Blood Sisters  kuisha.

Hivi utafanya nini endapo rafiki yako mpendwa kakuchukulia mpenzi wako? Hiki ni kionjo tu ndani ya Tamthilia ya The Lost Hearts, ambapo waigizaji nguli na wahusika wakuu wa tamthilia  hii Tessa na Magra ambao ni marafiki wakaribu sana wanakuja kua maadau kwa sababu tu ya mmoja wao anamsaliti mwenzake kwa kutembea na mpenzi wa mwenzie,hii tamthilia itatuonyesha namna inavyotesa kwa rafiki yako mpendwa kukuchukulia mpenzi wako.

Tamthilia kwa Ufupi
Tessa,ambaye ni  mbunifu wa mitindo na Marga ambaye ni malkia wa urembo na model, ni marafiki wa karibu wanaoshirikiana kutimiza ndoto zao licha ya ugumu wa maisha yao. Walakini, dhamana yao inapimwa wakati Caloy anaingia katika maisha yao. Caloy ana uhusiano wa kihistoria na Marga, lakini anapendelea kuweka mahusiano ya siri.
 Kisha Caloy akakutana na Tessa na wakapendana, ambapo wakasababisha Marga abadilishe uamuzi  wa kumrudisha kwake. Wakati huo huo, mahusiano ya Caloy na Tessa yanajaribiwa wakati Jaime, bosi wa Tessa na mjane wa marehemu ya Tessa, anapoanza kumpendelea.

Pamoja na hali ya wasiwasi kati ya marafiki na wapenzi inakua, bila kutarajia, maisha ya Caloy, Marga, Tessa na Jaime yanageuka ghafla na kua mwelekeo tofauti kutokana na kosa moja la ulevi. Baada ya hayo, kizazi chao kinaendelea kuchochea uhusiano bila kujua.
Kuendelea kupata uhondo huu wa Tamthilia ya The Lots Hearts Lipia kifurushi cha Mambo Tsh 14,000 Tu!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...