Katikati ni Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt,Aloyce Nziku akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Oldonyo Lengai ulipo katika kituo cha Kimataiofa cha Mikutano cha AICC Jijini Arusha leo 0ktoba 17,2019.kushoto kwake ni Agnes Kayoka ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uahirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika ya mashariki,Kulia kwake ni Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zamaradi Kawawa
Agnes Kayoka ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika ya mashariki
Na.Vero Ignatus -Arusha.
Tanzania inatazamia kuwa mwenyeji wa mkutano wa Mawaziri wa Sekta za mazingira ,Maliasili na Utalii wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC ambapo mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha AICC,Kuanzia Oktoba 21 hadi 25 mwaka huu 2019.
Dkt.Aloyce Nzuki ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii akifungua mkutano huo leo Oktoba 17,2019 Jijini Arusha amesema lengo la mkutano huo ni kuangalia mwenendo wa hali ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi,kubainisha utekelezaji wa mikakati ya hifadhi na usimamizi wa mazingira kupitia mkakati wa SADC,uchumi wa Bahari na kutathimini maendeleo katika sekta za misitu wanyamapori na Utalii.
Agnes Kayoka ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uahirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika ya mashariki amesema kuwa mikakati ya nchi katika Uenyekiti wa SADC ni kuhakikisha kuwa wanafanikisha matumizi ya lugha ya kiswahili kama lugha mojawapo katika nchi hizo 16 kwenye vikao vya SADC.
Kayoka amesema sambamba na hayo ni kuandaa kamati ya kitaifa ya kushughulikia maswala ya Jumuiya na Mtangamano.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 wananchama wa SADC wanaotekeleza mkakati wa SADC kuhusu usimamizi wa sheria juu ya vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori,programu za uhifadhi yaliyovuka mpaka wa nchi moja hadi nyingine kwenye maeneo ya misitu ,uvuvi,mazimgira na mabadiliko ya tabianchi,utalii,ukuzaji viumbe maji na mkakati wa ubora wa wanyama wa majini.
Aidha mkutano wa Mawaziri wa sekta za mazingira ,Maliasili na Utalii ni muendelezo wa mikutano itakayofanyika katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Tanzania ni mwenyeji wa Jumuiya hiyo.
Mkutano huo wa Mawaziri ,Maliasili na Utalii utatanguliwa na mikutano ya wataalam wa sekta ya wanyamapori utakaofanyika Oktoba 18 hadi 19 ambapo makatibu wakuu wa sekta za mazingira Maliasili utafanyika Oktoba 21 -24 ,2019 ambapo mikutano hiyo miwili itajadili mapendekezo yatakayowasilishwa katika kikao cha Mawaziri Oktoba 26 ,2019 kwa maamuzi na maelekezo.
Mapema mwezi Agosti mwaka huu, Serikali ya Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Dar es Salaam, Katika Mkutano huo,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikabidhiwa na kupokea rasmi jukumu la uenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ni moja kati ya jumuiya za kikanda katika bara la Afrika ambayo iliundwa kwa dhumuni la kuimarisha ushirikiano katika nyanja za uchumi, ulinzi, siasa na usalama,ambapo inaundwa na nchi wanachama 16 ambazo ni Angola, Botswana, Comoros,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Eswatini, Lesotho, Madagascar,Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Tanzania,Zambia na Zimbabwe.
Aidha Mkutano huo wa Mawaziri unatarajiwa kufunguliwa na Mhe.Samia Suluhu Hassani Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo mkutano wa Makatibu wakuu unatarajiwa kufunguliwa na Dkt.Hamis Kigwangalla ,Waziri wa Maliasili na Utalii 21Oktoba 2019 Jijini Arusha.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...