Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole (Katikati) akizungumza na wananchi wa Ujiji Mkoani kigoma leo na kukagua miradi ya maendeleo ya manispaa ya Kigoma Ujiji pamoja na Jengo la Mahakama ya Tanzania pamoja na Utandaji wa Mabomba ya Kusambazia maji.

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole  amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Mkoa wa Kigoma katika Manispaa ya Kigoma Ujiji leo.

Katika ziara hiyo Polepole ametembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Mahakama ya Tanzania ambalo limekamilika na litaanza kutumika hivi karibuni. Jengo hilo la Mahakama linakuwa sehemu ya utekelezwaji wa Ilani ya CCM inayotaka kusogezwa kwa huduma za utolewaji haki kwa wananchi na kuhakikisha haki za umma zinatolewa kwa wakati.

Ameihakikishia Mahakama kwamba Chama Cha Mapinduzi na Serikali wanataendelea kuiwezesha Mahakama ikiwamo ujenzi wa miundombinu  na nyenzo za kufanyia kazi.

Hata hivyo Polepole ametembelea na kukagua kazi inayoendelea Kigoma Ujiji ya Utandikaji wa mabomba na usambazaji wa maji katika magati yaliyo katika makazi ya wananchi pembezoni mwa mji wa Kigoma ujiji ikiwa ni sehemu ya kukamilisha mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Tanganyika.

"Huu ni muendelezo wa ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM inayotekelezwa na CCM chini ya Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Amesema polepole.

Polepole ataendelea na ziara yake Mkoani Kigoma na kuihitimisha kwa kutoa darasa la itikadi na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kwa Viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Kigoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...