CHAMA Cha Kuweka na Kukopa cha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA-SACCOS)  imefanikiwa katika utengenazaji wa mifumo ya Kisasa.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Nane wa TCRA Saccos LTD Afisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Omary Mkamba amesema anajivunia TCRA Saccos katika kwenda kisasa katika Manispaa hiyo.

Amesema kuwa katika ubora wa uendeshaji wa ushirika TCRA imekuwa ikifanya vizuri katika kwenda kisasa katika utoaji wa taarifa kwa wanachama ikilinganishwa na Saccos zingine.

Nae Mwenyekiti wa TCRA Saccos  LTD Erasmo Mbilinyi amesema Saccos imekuwa na mafanikio makubwa  ya kuwezesha kukopa kila mwanachama.

Mbilinyi amesema akiba za wanachama zimeongezeka kutoka zaidi ya sh.milioni 99 mwaka 2013 hadi kufikia sh.Bilioni 1.98 mwaka 2019.

Aidha amesema Hisa za wanachama  zimeongezeka kutoka zaidi sh.milioni 15 mwaka 2013 hadi kufikia zaidi ya sh.milioni 237 mwaka 2019.

Amesema madhumuni kuanzisha Saccos hiyo ni kuinua na kustawisha na kuboresha hali ya maisha ya wanachama ili kuweza kukidhi mahitaji mbalimbali ya kijamii na uchumi.
 Mwenyekiti wa TCRA Saccos LTD Erasmo Mbilinyi akizungumza katika mkutano mkuu wa nane wa wananchama wa TCRA Saccos  uliofanyika katika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Omari Mkamba akizungumza kuhusiana na Tcra saccos kujiendesha kisasa katika utoaji wa taarifa kwa wananchama wa saccos hiyo katika mkutano uliofanyika katika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Menejs wa Tcra Saccos LTD  Martin Kahimba akitoa maelezo kuhusiana na mwenendo wa Saccos katika mkutano mkuu wa Nane uliofanyika katika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam Rachel Magambo akizungumza kuhusiana maendeleo ya Saccos hiyo namna inavyofuata sheria  katika mkutano mkuu wa Nane uliofanyika katika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanachama wa Tcra Saccos wakiwa katika mkutano mkuu wa Nane uliofanyika katika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja watendaji wa Tcra Saccos pamoja na wageni walikwa katika mkutano wa Nane wa Tcra Saccos Ltd uliofanyika katika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...