Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KAIMU Mkurugenzi wa Idara ya Lishe kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Grace Moshi ametoa rai kwa wanaume wenye tabia ya kunyonya maziwa ya mama kuacha ili kuwapa nafasi watoto kupata lishe Bora kwa kunyonya ziwa la mama.

Hayo yametokana na mtindo wa baadhi ya  kinababa kulazimisha kunyonya maziwa ya mama huku watoto wakitoa lishe bora kutokana na kiwango cha maziwa kupungua.

Moshi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ikiwa  ni maandalizi ya mkutano wa mawaziri wa afya wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) ambapo amesema  mtoto ili awe na afya njema anahitajika kunyonya maziwa ya mama kwa miezi sita bila kila chochote.

"Mara kwa mara nimeona wakinamama wakilazimisha kuwapa uji au chakula kingine ikiwemo maji kwa Media maziwa haitoshi, hii si sawa lazima muelekeo maziwa ya mama ni chakula kilichokamilika," amesema Moshi.

Ametolea mfano waliokuwa katika ziara za kikazi kuhamasisha unyonyeshaji watoto wachanga, Moshi alisema waliwahi kupata maswali kutoka kwa wakinamama ikiwa maziwa yatawatosha watoto kwani waume zao wanalazimika ziwe moja Lowe la mtoto jingine la kwao.

"Msicheke hili, mnawezs kuona kama madhara lakini wapo kinababa wananyonya maziwa ya wake zao. Tusaidieni kuhamasisha ili hili lipungue," amesema na kuongeza mtoto anapozaliwa anatakiwa kunyonya maziwa ya mama tu kwa kipindi cha miezi sita bila kupewa kitu kingine ili kumfanya awe na lishe nzuri.

Kuhusu lishe nchini ,Moshi amesema kama nchini imepiga hatua kubwa katika eneo la lishe ukilinganisha na huko nyuma.

Ameongeza malengo yaliyowekwa duniani ni kwamba suala la lishe lisiwe zaidi ya asilimia 30 ambapo kwa Tanzania iko katika asilimia 32 ambayo ni juu ya lengo ambalo limewekwa katika eneo hilo la lishe.Hata hivyo amesema kwa Tanzania katika eneo la lishe ilikuwa na changamoto lakini kupitia mikakati ya Wizara imefanikiwa kupunguza ukubwa wa tatizo la lishe nchini.

Hata hivyo amesema kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha ukosefu wa lishe ambao unafanya kuwepo na udumavu na kwamba  kuna mikakati mbalimbali ya kutoa elimu ya kuhamasisha jamii kuzingatia suala la lishe.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Lishe kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Grace Moshi akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salam,wakati akieleza moja ya mada kuhusu wanaume wenye tabia ya kunyonya maziwa ya mama wanaonyonyesha Watoto wachanga,katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ikiwa  ni maandalizi ya mkutano wa mawaziri wa afya wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) unaotarajiwa kuanza Novemba 4-8,2019,ambapo Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.Picha na Michuzi JR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...