Baadhi ya mawakala wa Tigo Pesa hapa nchini wameeleza namna ambavyo wamekuza vipato vyao kupitia utoaji wa huduma ya Tigo Pesa huku wakiwataka watu kuchangamkia fursa hiyo. Mbali na huduma ya kutuma na kupokea pesa, huduma ya Tigo Pesa imekuwa huduma kamili ya kifedha ikitoa mikopo, bima, kuweka akiba pamoja na kupokea pesa kutoka nje ya nchi jambo linaloifanya kuongeza wigo wa fursa kwa mawakala wake.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti, Mawakala hao ambao wana uzoefu wa kati ya miaka mitano na saba kwenye huduma hiyo wamesema bado kuna fursa kupitia huduma hiyo inayokua kwa kasi hapa nchini. Suleiman Hussein kutoka visiwani Zanzibar ambaye amefanya kazi ya uwakala kwa kipindi cha miaka saba anasema kuwa kupitia Tigo Pesa ameweza kuimarisha kipato chake kwa kiasi kikubwa ikiwamo kumuwezesha kununua gari mbali na kuendesha familia yake. 

 “Nashukuru Mungu kupitia Tigo Pesa kipato changu kimekua na nimeweza kununua gari langu pamoja na kuendesha familia yangu.Naona kuna fursa kubwa sana kwenye huduma hii ya Tigo Pesa na ndio maana naendelea kukuza mtaji wangu, kuhudumia wateja wengi zaidi kwasababu ni huduma inayohitajika kila siku,” alisema Hussein.

 Hussein anawahimiza mawakala kuboresha zaidi utoaji wa huduma ili kuweza kuvutia wateja.Pia, aliwataka wateja kutumia zaidi huduma za Tigo Pesa katika shughuli zao za kila siku. Naye, Vicky Ibrahim wakala wa Tigo Pesa katika maeneo ya Kariakoo – Msimbazi anasema tangu ameanza kazi hiyo ya uwakala miaka mitano iliyopita ameona mabadiliko makubwa kiuchumi licha ya kuanza na mtaji kiduchu.

 “Nilianza na mtaji mdogo sana wa laki sita (600,000/-) ila kwa sasa namshukuru Mungu umezidi kukua siku hadi siku.Kuna mafanikio mengi sana nimezidi kuyapata katika kazi zangu kwanza familia yangu imezidi kunufaika kwa kiasi kikubwa.” Anasema siri kubwa ya ukuaji huo ni utoaji wa huduma zenye kuzingatia uaminifu na ubora kwa wateja jambo ambalo linawafanya kuzidi kufika katika ofisi yake. “Wale ambao wanatarajia au wanataka kuwa mawakala nawakaribisha kwa mikono miwili kwani mimi nilianza na msingi mdogo sana lakini saizi nimepata mafanikio makubwa kupitia hii kazi ya uwakala wa Tigo Pesa,’ alisema. 

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha anasema kuna fursa nyingi zinazopatikana kupitia uwakala wa Tigo Pesa kwakuwa kwa sasa huduma hiyo imekuwa huduma kamili ya kifedha. “Tigo Pesa ilianza kama huduma ya kutuma na kutoa pesa ila kwa sasa ni huduma kamili ya kifedha tunatoa mikopo,tunatoa bima ya matibabu kwa mtu na familia na pia tunawawezesha wateja wetu kuweka akiba.Pia, tunawezesha makampuni kufanya malipo mbalimbali kwa urahisi na usalama zaidi,” anasema Pesha. 

Pia, huduma ya Tigo Pesa imeingia katika huduma za fedha kidigitali kupitia App ya Tigo Pesa ambayo inampa mteja uwezo wa kutuma na kupokea pesa na pia kurudisha muamala uliokosewa kwa urahisi zaidi. “Napenda kuwahamasisha mawakala wetu kuendelea kufanya kazi na Tigo kwani fursa bado ni nyingi na pia tunaendelea kutafuta mawakala na kwa wateja wetu waendelee kufanya miamala na Tigo kwani Tigo Pesa ni zaidi ya Pesa,” alisema Pesha. Mwisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...