VICTOR MASANGU, PWANI
SHIRILA la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) katika kukabiliana
na changamoto ya uagizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi imekuja na
mpango kabambe wa miradi mikakati mitatu kwa ajili ya kufanya
utafiti wa uchimbaji wa visima vya mafuta katika mikoa ya
Tabora,Simiyu, pamoja na singida lengo ikiwa ni kuipunguzia serikali
ya awamu ya tano kutumia gharama kubwa katika suala zima la
uagizaji.
Hayo yalibainsihwa na Afisa Mahusiano ya jamii wa TPDC Eugene Isaya
wakati wa maonyesho ya bidhaa za wawekezaji wa viwanda katika Mkoa
wa Pwani, ambapo pia amebainisha kuwa lengo lao linguine ni kuweza
kutanua wigo katika kuzalisha gesi asilia katika maeneo mbali mbali
nchini ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi kuondokana na
mtumizi ya ukataji wa miti ovyo.
Kwa upande wake Afisa uhusino wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC)
Latipher Kigoda amesema kwamba lengo kubwa ni kuwasimamia na
kuwaunganisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ikiwemo kutanagaza
fursa mbali mbali zilizopo kwenye kilimo pamoja na kuongeza thamani
katika mazao ya biashara sambamba na kuwa na vifaa tiba ambavyo
vinazalisha ndani ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye
amepokea jopo la wawekezaji saba Kutoka jimbo la hebeyi kutoka
nchini na kuwakabidhi mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa ambao utaweza
kuonyesha fursa mbali mabli ambazo zinapatikana katika halmashauri
zote tisa lengo ikiwa ni kuwapatia maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa
kuzalisha chuma,nondo na saruji.
Afisa Mahusiano ya jamii wa TPDC Eugene Isaya akizungumza
na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa maonyesho ya bidhaa
kwa wawekezaji wa viwanda Mkoa wa Pwani (PICHA VICTOR MASANGU)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...